July 12, 2017

WANAKIJIJI NYAZWA WAMWOMBA MBUNGE MWAMOTO AWALETEE RAIS DKT MAGUFULI

Mwenyekiti  wa  kijiji  cha Nyanzwa  akifungua mkutano  wa  mbunge
Mbunge  Mwamoto  kushoto  akikabidhi  vifaa vya  michezo  kwa  madiwani wake
Wananchi  wakiwa  katika mkutano  wa mbunge

Mbunge  Mwamoto  akiwahutubia wananchi  wa  kata ya  Nyanzwa
Wanawake  wakiwa wamekaa katika  ndoo  kumsikiliza  mbunge  wao
Na  MatukiodaimaBlog
WANANCHI wa  kata ya  Nyanzwa  wilaya ya  Kilolo mkoa  wa  Iringa  wamwomba mbunge wa  jimbo la Kilolo  Venance Mwamoto kumwomba  Rais  Dkt John Magufuli kufika  katika  kata  hiyo  ili  waweze kumwona  na  kumpongeza kwa  kazi nzuri anayoifanya ya  kupambana na  vita  ya uchumi   katika Taifa .

Wakizungumza jana wakati wa  mkutano  wa mbunge wao  kutoa mrejesho wa kile walichomtuma  bungeni  wananchi hao  walisema kuwa  wamepata  kuwa kazi anayoifanya  Rais Dkt  Magufuli ni kazi ambayo imerejesha imani ya serikali kwa  wananchi wote  pasipo kujali  vyema  vyama na  kuwa  wanatamani kuonana na Rais katika  kata  yao ili  kumshuhudia  kwa  sura  na  kumpongeza .

“Wamepita marais wengi  ambao  tumekuwa  tukiletewa mabango na  tumekuwa  tukiwachangua bila kuwaona kwa sura ila  hakuna siku tuliomba  kuonana na Rais ila kwa  huyu wa  sasa   tunaomba   sana mbunge  wetu pamoja na kuwa hakuna  ulipoahidi  kutuletea Rais  ila  sisi kama  wapiga kura  wako  tuliokuchagua tunaomba  utuletee Rais  Magufuli “alisema  John Mbwale

Kuwa wao kama  wananchi  wa kata ya  Nyanzwa  wamekuwa  wakifuatilia  kazi na  utendaji  wa  mbunge  wao Mwamoto  na Rais na  kuona kuwa kazi  hizo  zinawavutiwa na  kuona  kuna haja ya  kukutana  ana kwa ana na  Rais  ili  kuweza  kumpongeza kwa  kuyatekeleza  kwa  vitendo yale  yote  aliyoahidi  wakati wa kampeni.

Aidha  wananchi hao  walisema  kero  yao kubwa katika kata  hiyo ambayo  wananchi wake  wanaishi kwa  kutegemea  kilimo cha  umwagiliaji ni  kupata  bwawa  la  kuendeshea  kilimo   hicho  huku  wakimpongeza mbunge  wao  kwa  kutekeleza ahadi yake ya  mawasiliano ya  simu kama  alivyoahidi  .

“ Mheshimiwa  mbunge  kwa  upande  wako  sisi  kweli  tunakupongeza wewe ni mkweli ulituahidi  kupata  mawalisiano ya  simu  leo  hii  tumepata  hata kabla ya  miaka  yako  mitano  kumalizika  ila tulikuwa na mbunge  miaka 10 alituahidi mawasilano hadi anaondoka  alituacha  kama  alivyotukuta …..sisi  tunakuona  wewe  ni  mchapa kazi kama rais Magufuli tunaomba  Mungu awabariki  sana “

Kwa upande  wake  mbunge  Mwamoto pamoja na kuwashukuru  wananchi hao  kwa kutambua  kazi nzuri  inayofanywa na Rais Dkt Magufuli na serikali  yake  CCM bado alisema lengo la  serikali ni  kuona  wananchi  wanapata  maendeleo na  kuondokana na kero  zisizo  za msingi na ndio  maana   katika bajeti ya  mwaka
2017/2018  serikali  imefuta  tozo  mbali  mbali  ambazo  zilikuwa kero kwa wananchi  zikiwemo  za mazao.

Alisema kuwa  serikali iliyopo madarakani  ni  serikali ya kazi  na  sio  ya  maneno  bila kazi  hivyo alisema sababu ya  kuzuia  maandamano na mikutano ya  mbunge  mmoja kwenda  mkoa mwingine ni kutaka  wabunge  wafanya  kazi kwa wananchi katika maeneo yao  na  sio  kufanya mikutano  isiyo na  tija kwa maendeleo .

Mwamoto  alisema suala la  kero  ya  bwawa la umwagiliaji na maji  safi kwa wananchi wa Nyanzwa  lipo  mbioni kutekelezwa na kabla ya  kuondoka madarakani bwawa  hilo  litakuwa  limejengwa  kwani hadi  sasa  serikali imetenga  bilioni 5  kwa  ajili ya bwawa  hilo kijiji  cha  Nyanzwa .

Kuhusu  umbi la  wananchi  hao  kutaka  kumwona Rais  katika  kata   hiyo  alitaka  wananchi hao  kuanza ujenzi wa kituo  cha afya  kwenye kata  hiyo ili anapokuja afanye kazi ya  kuzindua  kituo  hicho  na  sio kuja kwa ajili ya kutembea .
Alisema kwa  kuwa   wananchi hao  wanatamani  kukutana na  Rais  basi  wanapaswa  kushirikiana pamoja  kujenga  kituo  cha afya haraka  ili anapokwenda  kumomba  Rais  kufanya  ziara  kata  hiyo  basi  kuwe na mradi   wa  kuzindua ambao  ni kituo  cha afya .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE