July 26, 2017

WANAFUNZI WA MGAMBO MAFINGA WACHANGIA DAMU UNITI 30 HOSPITALI MAFINGA

WANAFUNZI wa mafunzo ya Mgambo  katika mji  wa Mafinga  wilaya ya Mufindi mkoani Iringa  wamechangia Unity 30  za damu katika Hospitali ya  wilaya ya Mufindi  kwa  ajili ya  kusaidia akiba ya damu  zaidi Hospitalini hapo .

Akiwapongeza  kwa  uchangiaji wa damu  hiyo  mkuu  wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza  jana alisema kuwa  uhamasishaji  uliofanywa na wanafunzi hao  wa mgambo katika mji  wa Mafinga katika kuchangia damu  unapaswa  kuwa  endelevu  kwa  wananchi  wengine  kuendelea  kujitolea damu .

Mkuu  huyo  wa mkoa  alisema  uchangiaji  damu  huo unaokwenda  sambamba na maandalizi ya  wiki ya mashujaa iwapo utafanywa na wananchi  wengine  wa wilaya ya Mufindi na mkoa mzima  utasaidia  kupunguza changamoto ya  damu katika kituo  cha ukusanyaji wa damu  salama   kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa  wa Iringa.
0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE