July 18, 2017

WAKENYA WATAKIWA KUTOKUFANYA MAPENZI AGOST 7 MWAKA HUU

Mgombea Urais nchini Kenya kwa tiketi ya Umoja wa Upinzani (NASA), Raila Odinga amewataka wananchi nchini humo wasifanye mapenzi na wenza wao usiku wa Agosti, 7 mwaka huu.
Odinga ameyasema hayo wakati akihutubia katika eneo la Homa Bay ambapo alisema wananchi wanatakiwa kujiandaa kwa uchaguzi ambao utafanyika Agosti, 8 na hivyo ni vyema siku hiyo wasikutane na wenza wao ili wajiandae kwa uchaguzi.
Katika kusisitiza hilo amewataka hata ambao wapo kwenye ndoa kufata ushauri wake na akiwataka wanawake kuwanyima waume zao unyumba hata kama wakitaka kufanya nao mapenzi.
“Tunakwenda kwenye vita tunahitaji kuwa na nguvu ya kutosha kabla hatujaingia kwenye vita Agosti 8, hakuna mtu kati yetu anatakiwa kufanya mapenzi usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi,
“Wanawake wote wanapaswa kuwanyima waume zao haki yao kwa usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi,” alisema Odinga wakati akiwahutubia wananchi na kuongeza.
“Tukifanya hivyo tutaweza kuamka mapema, tutapiga kura na tutakuwa vizuri mpaka siku matokeo yanatangazwa.”

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE