July 12, 2017

WAFUGAJI WALALAMIKA KWA MBUNGE MWAMOTO WADAI WAMEVAMIWA .....

Wafugaji  jamii ya  kimasai  wakazi wa Ruaha mbuyuni  wilaya ya  Kilolo  wakiwa  wamedandia gari ya  mbunge Mwamoto  baada ya  ndani  kujaa wakielekea  kuonyesha kero  zao na wakulima
gari ya  mbunge haijai
mbunge  wa  jimbo la Kilolo Venance Mwamoto katikati  akiwa na viongozi wa  jamii ya  kimasai 
..........................................................................................
Na matukiodaimaBlog 
WAFUGAJI  jamii ya  kimasai  wakazi  wa  kijiji  cha Ruaha  Mbuyuni wilaya ya  Kilolo  mkoani  Iringa wamlalamikia mbunge  wa  Kilolo Venance  Mwamoto baada ya  eneo  lao  kuanza  kuvamiwa  na  wakulima  kwa  kufanya  shughuli  za  kilimo katika eneo lao la malisho.

Wakizungumza  jana  wakati wa  sherehe ya vijana wa  kimasai kijijini  hapo  wafugaji hao  walisem a kuwa  eneo  hilo  lilitengwa  maalum kwa ajili ya wafugaji   ila  kwa sasa wananchi wameanza kusogea  taratibu kwa  kufanya  shughuli  za  kilimo  jambo  ambalo wanaliona kama ni mwanzo  wa  mgogoro  kati  ya  wafugaji na  wakulima.

Hivyo  walimuomba  mbunge Mwamoto  kufikisha  malaalamiko yao  hayo kwa  uongozi wa Halmashauri  ya wilaya  ya  Kilolo  ili  kufika  eneo hilo kwa  ajili ya  kuweka mipaka  na  kuchukua hatua  za  haraka  kuepusha  migogoro inayoweza  kutokea mbeleni  alisema mmoja kati ya waafugaji hao  Ally Sayuhu kwa  niaba ya  wenzake .

Kwani  alisema kuwa  kijiji  hicho  kina  viongozi  wa  serikali ya  kijiji  ila wamekuwa  wakilifumbia macho suala hilo la wafugaji  kuvamiwa maeneo  yao huku pindi wakulima  wakiwa na malalamiko  yao  juu ya  wafugaji  viongozi  hao  wamekuwa  wepesi  zaidi  kufika na kuchukua hatua.

Alisema  kuwa  eneo la  wafugaji kunyweshea  maji mifugo  yao  lipo na  lina maji ya  kutosha  ila  tatizo  ni wakulima  kulima jirani na  eneo hilo   hivyo  imekuwa vigumu kwao  kupitisha  mifugo  kwenda katika eneo la maji  kutokana na njia ya  kupitisha   mifugo  kulimwa mazao.

Kwa  upande  wake mbunge  Mwamoto  alisema kuwa  malalamiko  hayo atayafikisha   ofisi ya  mkurugenzi wa Halmashauri  hiyo  ili  kuleta  wataalam wake kwa  ajili ya  kumaliza kero   hiyo kati ya  wafugaji na  wakulima .

Huku  akiwataka  kutenga  eneo ambao  wao  wanaona ni rafiki  zaidi kwako  kutumia kunyweshea  mifugo  yao  na  yeye atasaidia  kuleta  wataalma na  kufanya mkutano ili  kila mmoja ajue  wajibu  wake .

Mbunge  huyo  alisema  suala  la  elimu  kwa  wafugaji  hao  linahitajika  ili  kuongeza  thamani ya mazao  ya mifugo yao kwa maana ya kuwa na mifugo bora na maziwa  yaliyoboreshwa  badala ya  kuendelea  kufunga mifugo mingi isiyo  bora .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE