July 4, 2017

WABUNGE WA CHADEMA WALIOTAKA KUMPIGA MBUNGE WA CCM JULIANA WAKAMATWA

Mbunge Juliana Shonza


Habari  kutoka  mjini Dodoma  zinaeleza  kuwa  wabunge kadhaa  wa  chama  cha  Demokrasia na maendeleo  (CHADEMA) ambao  walikwazika  na  uchangiaji  wa mbunge  wa  CCM Juliana  Shonza  na  kutaka kumpiga  wakati  mbunge  wa Kawe  Halima  Mdee  alipokuwa  akipewa adhabu  kwa  kutoa  lugha  chafu  bungeni wamekamatwa .


Taarifa zilizoufikia mtandao  huu wa matukio daima  zinadai kuwa wabunge  hao   walikamatwa jana  majira  ya  usiku baaada ya  bunge kuarishwa  na baada ya  kukamatwa  walifikishwa  polisi  na bado  haijajulikana  iwapo  waliachiwa ama  lah.

Idadi  ya  wabunge  waliokamatwa  inasadikika  kufikia zaidi ya  watano ,mtandao   huu  unaendelea  kumtafuta  kamanda  wa  polisi mkoa wa Dodoma  ili  kuthibitisha  kukamatwa  kwa  wabunge  hao.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE