July 24, 2017

UGONJWA WA AJABU UNAVYOWATESA WANAFUNZI TANGAWANAFUNZI wanaosoma shule ya sekondari ya Kwamkabara kata ya Kwamkabara wilayani Muheza mkoani Tanga wamepatwa na ugonjwa wa ajabu unaosababisha kuanguka hovyo,
Ugonjwa huo umesababisha wanafunzi 52 mpaka 70  wanaanguka baada ya kushikwa na ugonjwa waajabu wa kuanguka na kupiga kelele pamoja na kutokwa ute mdomoni kama wamepandisha mashetani.
Tukio hilo limetokea juzi katika shule hiyo ya sekondari ya kata ya Kwamkabara wilayani Muheza mkoani Tanga. Mkuu wa shule hiyo Getrude Moyo amethibitisha kuwapo tukio hilo la watoto kuanguka na kupiga kelele.
Akizungumza eneo la tukio Ofisa elimu wa shule za msingi wilayani Muheza, Julitha Akko amesema kuwa wanafunzi hao walishikwa na ugonjwa wa kuanguka na kupiga kelele kama wamepandisha mashetani.
Akko alisema kuwa mpaka sasa chanzo cha wanafunzi hao kuanguka na kupiga kelele bado hakijafahamika na wazazi kwa kushirikiana na walimu wa shule hiyo walifanya maombi ya kukemea mapepo  katika shule hiyo na baadae wanafunzi hao kuchukuliwa na kurudi nyumbani.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE