July 26, 2017

UCHOVU WA SAFARI ,LIPULI YANYUKWA 4-0 NA AZAM FCUchovu  wa  safari kutoka  Dar  es Salaam  kuja  Iringa siku moja kabla ya mchezo  wake wa kirafiki wa   kwa  timu ya   soka la Lipuli  Fc ya  mkoani Iringa ambayo  iinajiandaa  kwa  mchezo  wake  wa ufunguzi  wa  ligi  kuu Tanzania  bara na  timu ya  Yanga  Afrika imepelekea Lipuli Fc kushindwa kujipima  nguvu na  timu ya Azam Fc  baada ya  kukubali  kichapo cha magoli 4-0 katika  uwanja wake wa nyumbani .
Katika  mchezo  huo  wa kirafiki kwa ajili ya timu  hiyo ya  Lipuli Fc na Azam Fc kujiandaa kwa ligi  kuu  uliopigwa  leo kwenye  uwanja wa Samora  mjini Iringa  na  kushuhudiwa na mamia  ya  mashabiki  wa  Lipuli Fc  wakiongozwa na  viongozi mbali mbali wa  serikali mkoa wa Iringa ,timu ya  Lipuli Fc ilionekana si  ridhiki katika mchezo  huo kwa  kukubali kichapo  hicho .
Lipuli Fc ambao  muda wote  walifanikiwa kulifikia lango la Azam Fc bado  walioonyesha  kuwa na  uwezo mdogo wa  kuziona nyavu  za Azam Fc hivyo kuishia  kupiga  mashuti  yasiyo na mafanikio .
Wadau  wa  soka  mjini  Iringa mbali ya  kuelezea furaha  zao  kwa  kuanza kuonja  raha za  ligi  kuu  ila bado walidai  kuwa  timu  hiyo  kufungwa  ilikuwa ni haki yake kwani  imetumia  muda  mwingi kuvutana  zaidi badala ya  kufanya  usajili  na hivyo  kutaka  viongozi  waliochaguliwa  kuongoza  timu  hiyo  kuweka mikakati ya kuiondoa timu katika aibu ya  kufungwa siku za mbeleni  alisema Khamis  Juma .

Kuwa  lazima  viongozi wa  Lipuli Fc  kufanya kazi  kubwa ya  kuisuka  timu  hiyo ili  mchezo  wake wa ufunguzi wa Ligi  kuu na  Yanga  kufanya vizuri  zaidi ila  sio  kukubali  kuendelea  kupokea kichapo kama hicho.

“Timu  yetu ya  Lipuli Fc kweli imetia aibu  wenzetu Njombe wameweza kuwafunga  Azam kwa  jumla ya goli 2-0  ila  Lipuli Fc  tunachapwa mara  mbili yake hii ni aibu na  ni somo kwa viongozi wa Lipuli Fc kujipanga kwa  michezo ijayo ili  isije kuwa ni  wasindikizaji wa ligi kuu “

Katika  mchezo  huo wa kirafiki Azam  Fc  iliweza  kujipatia magoli mawili  kipindi  cha kwanza na magoli mawili  kipindi cha pili  magoli yaliyofungwa na mchezaji  Yakubu Mohamed , waziri Junio  ,Yahaya  Mohamed na Shua Boy .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE