July 24, 2017

TRA IRINGA YAANZA KUFUNGA BIASHARA ZOTE AMBAZO HAZINA MASHINE ZA EFDs ,IRINGA

Wananchi  wa  Iringa wakitazama maduka  yaliyofunga  na  TRA  eneo la  Miyomboni mjini Iringa  leo  maduka hayo yamefungwa   kwa  kukosa mashine za EFDs
Baadhi ya maduka mjini Iringa yakiwa yamefungwa leo
kaimu  meneja  wa TRA mkoa  wa Iringa Lamsony Tulianje akizungumza na matukiodaimaBlog
Wakala  wa mashine za EFDs  Iringa Himid Mbata  akihudumia  wateja 
wateja  wakiwa katika  foleni ya kununua mashine za EFDs  leo 

.............................................................................................................................................
Na Matukiodaimablog
MAMLAKA  ya  mapato Tanzania  (TRA)  mkoa  wa Iringa  imesema itaendelea  kufunga  maduka  na biashara  zote  mkoani Iringa ambazo  hazitakuwa na mashine  za kieletroniki za  EFDs  iwapo  kwa  wale  wasio na mashine   hizo .

Kaimu  meneja  wa RTA  mkoa wa Iringa Lamsony Tulianje  akizungumza na wanahabari  jana  ofisini  kwake  alisema  kuwa zoezi  hilo la kufunga  biashara  mbali mbali  limeanza  kwa kasi kubwa na kuwa zoezi hilo  litaendelea  katika maeneo yote ya  mkoa wa Iringa .

Alisema  kuwa  biashara  zote  zinapaswa  kuwa na mashine  hizo na mfanyabiashara  asiye na mashine  hiyo biashara  yake  itafungwa na  hivyo  kutoa  wito kwa wafanyabiashara  kutekeleza agizo hilo haraka  iwezekanavyo kwani  muda wa  kuwa na mashine  hiyo  bila  shuluti  umekwisha.

Hata  hivyo  kwa upande wao  wafanyabiashara  ambao   biashara  zao  zimefungwa na TRA leo katika msoka  unaoendelea   walisema  kuwa  baadhi yao  walikwisha  lipia  pesa kwa  ajili ya  mashine  hiyo  kupitia mawalaka  ambao  waliteuliwa na  serikali ila toka mwaka  2014  hadi sasa  hawajapewa mashine  hizo.

Hivyo  walitaka  serikali ambayo  ndio  iliwaleta  mawakala  hao  kuwasaka  ili  kurejesha  fedha  zao ama kuchukua  hatua  stahiki dhidi yao .

Mmoja kati ya mawakala  wa mashine  hizo Himid Mbata  alisema kwa upande wake  ni wakala wa kampuni ya Adva Tech  ila hakuna mteja ambae  alipata  kulipia mashine  hizo kwake hajapata na kuwa  kutokana na baadhi ya mawakala  kutotimiza  wajibu wao  hivi  sasa kumekuwa na msongamano mkubwa katika ofisi yake  kutaka kununua mashine  hizo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE