July 27, 2017

RC IRINGA -NITAZISHITAKI BANK KWA RAIS MAGUFULI..

Wadau wa ushirika wakieleza mafanikio
Mwakilishi wa Mazombe Sacco's 
Mwakilishi wa CRDB Iringa

MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza atishia kuzishitaki bank mkoani hapa kwa Rais Dkt John Magufuli iwapo zitaendelea kuwa kikwazo kwa vyama vya ushirika mkoani hapo.

Mkuu huyo wa mkoa aliyasema hayo jana
wakati wa ufunguzi wa jukwaa la ushirika
mkoa katika ukumbi wa siasa ni Kilimo mjini Iringa ,kuwa moja kati ya sababu kubwa zinazochangia vyama vya ushirika vingi mkoani Iringa kuyumba ni kutokana na taasisi hizo za kifedha kama Bank kushindwa kutoa elimu na ushauri kwa vyama vya ushirika kabla ya
kuvipa mikopo na badala yake vyama hivyo
kuyumba kutokana na mikopo kandamizi inayotolewa .

“Na mjue huko tunakokwenda mimi hizi bank zenu nitazishitaki kwa mheshimiwa Rais Dkt John Magufuli ninyi mnatakiwa kuwa wawazi
zaidi mmekuwa mkiingia mikataba ya vyama vya ushirika huku mkijua hawajui chochote juu ya mikataba hiyo na mwisho wa siku
mmekuwa mkichangia vyama hivyo
kufa”alisema Masenza
Kuwa bank zinapaswa kuhakikisha zinaingia mikataba na vyama vya ushirika baada ya
kuwapa elimu na iwapo wataona chama husika hakina elimu juu ya mkataba husika ni
vizuri kwenda Halmashauri na kukutana na wataalam wa sheria kwa niaba ya chama cha ushirika ndipo waweze kuingia mikataba na si
vinginevyo.

Alisema kitendo cha taasisi za kifedha kuingia
mikataba bubu na vyama vya ushiriki huku
wakitambua wazi kuwa mkataba huo utaleta
shida kwa wahusika ni kuwakandamiza na sio
kuwasaidia hivyo iwapo taasisi hizo za
kifedha hazitabadilika atazishitaki kwa Rais .
“ kuna chama kinaitwa Itukoje kimeweza
kuingia mkataba mbovu na moja kati ya bank zetu zilizopo hapa mkoani na mkataba huo unaendelea kuwatesa wanachama jambo ambalo mimi kama mkuu wa mkoa sijapenda mikataba ya aina hiyo kuendelea kuingiwa na vyama vya ushirika”

Hivyo alitaka bank ndani ya mkoa wa Iringa
kutambua kuwa zipo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Tanzania na sio kujinufaisha kwa mikataba mibovu kupitia watanzania hao na
iwapo kila bank itasimama kwa ajili ya kumsaidi mtanzania malengo ya serikali ya
kuwakomboa watanzania yatafanikiwa .

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa tawi la CRDB Iringa Kissa Samwel ,m wakilishi wa bank ya CRDB Iringa Ashery Mwenda ambae
ni meneja wa mahusiano alisema kuwa
ushauri uliotolewa na mkuu wa mkoa juu ya bank kuwasaidia wananchi watalifanyia kazi ili kuona kero kama hizo haziendelei kujitokeza .

Kuwa bank yake imeendelea kuwa
kiunganishi sahihi kwa wanaushirika ndani ya mkoa wa Iringa kwa kuwatunzia fedha zao kwa usalama pamoja na kuwapa mikopo mbali mbali na mafunzo kwa wanaushirika na misaada vya vitendea kazi.

Awali kaimu mrajisi msaidizi mkoa wa Iringa
Fausta Kasuga alizitaja changamoto mbali mbali za ushirika kuwa ni pamoja na kuwepo kwa vyama vingi sinzia, ukosefu wa elimu ya
kutosha ya ushirika,kuwepo kwa ubadhirifu
kwa baadhi ya vyama vya ushirika,vyama vya ushirika kuwa na madeni makubwa hasa katika vyama vya ushirika wa wakulima wa tumbaku
pamoja na ukosefu wa maafisa ushirika katika Halmashauri za wilaya na Manispaa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE