July 17, 2017

PROGRAM YA TUSEME IWE MKOMBOZI KWA UKATILI IRINGA -RC MASENZA

wanafunzi wakionyesha burudani 
Wadau wakiwatuza wanafunzi watoa burudani 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wa tatu kushoto akiwa na wadau wa elimu mkoa 
Mkuu wa mkoa wa Iringa akipokelewa 
Wanafunzi 300 walioshiriki wakiingia ukumbini 
Mratibu wa Tuseme mkoa wa Iringa Kenneth komba akielezea mradi huo 
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam akimkaribisha mkuu wa mkoa 
............................................................
Na Matukiodaimablog 

MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ametaka program ya Tuseme kwa wanafunzi wa shule za msingi katika mkoa wa Iringa isaidie kukomesha vitendo vya ubakaji na uanzishwaji wa lishe mashuleni .

Akifungua tamasha la mwaka la Tuseme katika ukumbi wa JKT Mafinga leo mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa pamoja na kazi mbali mbali zinazofanywa na Tuseme katika kuwalinda watoto majumbani na mashuleni bado kuna haja ya shule kuanzisha utaratibu wa kutoa chakula kwa wanafunzi wa shule za msingi. 

Alisema kuwa kufanyika kwa tamasha hilo la wadau wa elimu na wanafunzi iwe ni fursa ya kipekee ya kuongea na wadau hao wa elimu katika mkoa kuona watoto wanalindwa na hata kuanzishiwa chakula mashuleni. 

"Napenda kushukuru shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto duniani (UNICEF) Kwa kusaidia kufadhili Program mbali mbali za elimu katika mkoa wa Iringa... Mkoa wetu wa Iringa unapongeza UNICEF kwa kuanzisha program hii ya Tuseme ambayo ambayo itasaidia kuwajengea uwezo wanafunzi wa shule za msingi "

Kwani alisema kwa kupitia program hiyo wanafunzi wa shule za msingi wataweza kuongea kwa uwazi masuala yanayohusu ustawi wao mbele ya wadau wa elimu na jamii nzima kwa ujumla. 

Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa kuwa program hiyo inawawezesha wanafunzi kuibua masuala mtambuka, kuishauri serikali na wadau mbali mbali wa elimu kuhusu uboreshaji wa mazingira yao ya kufundishia na kujifunzia anaamini itasaidia kuongeza kiwango cha elimu kwa mkoa.

Hivyo alisema kupitia program hiyo jamii itaelimishwa juu ya lishe bora kwa watoto pia elimu ya kuzuia ukatili kwa watoto na matukio ya ulawiti na ubakaji. 

Alisema changamoto mbali mbali zinazowakabili watoto kwa kupitia Tuseme zitaweza kutatuliwa na kuboresha elimu kwa wanafunzi mkoani Iringa. 

Hivyo alishauri shale zote kuanzisha vikundi vya Tuseme kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kupaza sauti zao wanavyofanyiwa vitendo vya kikatili. 

Mratibu wa Program ya Tuseme mkoa wa Iringa keneth Komba alisema program hiyo kwa sasa imeanzishwa katika halmashauri zote za mkoa wa Iringa japo awali ilianza katika wilaya ya Mufindi na kuna mafanikio makubwa yamepatikana. 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE