July 23, 2017

RAMADANI MAHANO MWENYEKITI MPYA KLABU LIPULI FC

Mwenyekiti mpya wa klabu ya soka ya Lipuli FC Ramadhan Mahano akiomba kura leo 
Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Lipuli FC 
Mwenyekiti mpya wa Lipuli Fc Ramadhan Mahano alipokuwa akiomba kura 
Abuneri Mrema aliyekuwa akigombea nafasi ya kiti Lipuli FC 
Hawa wote ni wajunbe wa Klabu ya Lipuli FC 
Wajumbe wa mkutano mkuu wa Lipuli FC wakipiga kura 
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Abudalah kushoto akisimamia uchaguzi wa Lipuli FC leo 
Mrema akipiga kura 
mwenyekiti mstaafu Lipuli FC Abuu Changawa akipiga kura leo kuchagua mrithi wake 
mjumbe Luca Kambanyuma akipiga kura 
Mjumbe Husna Ngasi akipiga kura 
Mjumbe Kalinga akijipigia kura 

Mnyinga akijipigia kura leo  


Victor Chakudika mmoja kati ya viongozi wa kikundi cha hamasa cha Hamsha Popo akipiga kura leo  
Mwenyekiti mpya wa Lipuli FC Ramadan Mahano wa tatu katika mstari akijiandaa kwenda kupiga kura leo 
Wajumbe wa mkutano mkuu wa Lipuli FC wakipiga kura Leo 

Na MatukiodaimaBlog 
WANACHAMA wa klabu ya soka ya Lipuli Fc ya mkoani Iringa leo wamemchagua Ramadhan Mahano kuwa mwenyekiti mpya wa klabu hiyo baada ya kuwagalagaza wapinzani wake wawili. 

Katika uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Shule ya sekondari Mwrmbetogwa na kushuhudiwa na mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ambae aliwakilishwa na mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah jumla ya wajumbe 172ndio wameshiriki mkutano huo mkuu wa uchaguzi. 

Akitangaza matokeo hayo ya uchaguzi huo Wakili Jackson Chakula alisema kuwa Mahano ameshinda kwa kura 103.

Wakati mpinzani wake Nuhu Mnyinga akimfuata kwa kura 60 wakati Abuneri  Mrema akipata kura 4.

Huku makamu mwenyekiti ambae aligombea nafasi hiyo pekee yake Abuu Kihwere akishinda kwa kura 116 huku kura 56 zikiharibika 

Wajumbe  wote watatu kati ya wanne waliokuwa wakitakiwa wamepita katika nafasi hiyo wajumbe hao ni Renatus Kalinga, Servesta kanyika
na Magid Matolla 

Awali mgeni rasmi katika mkutano huo mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abudalah aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuchagua viongozi watakao ifanya Lipuli kusonga mbele na sio viongozi wa kuendekeza migogoro na kurudisha nyuma Lipuli. 

Alisema kwa kupitia Lipuli Fc mkoa wa Iringa utaweza kupiga hatua ya kimaendeleo katika sekta mbali mbali ikiwemo sekta ya utalii katika hifadhi za Udzungwa, Uzungwa, Hifadhi ya Mazingira ya asili Kilombero, hifadhi ya Milima ya Uzungwa na hifadhi ya Taifa ya Ruaha na maeneo mengine mengi ya utalii mkoa wa Iringa. 

Hivyo alitaka viongozi wa soka kuwa wamoja ambao wataiwezesha timu hiyo kufanya vizuri zaidi. 

Kwa upande wake aliyekuwa mwenyekiti wa Lipuli FC Abuu Changawa alisema amepisha uchaguzi huo yeye na wenzake ili timu hiyo kusonga mbele na iwapo watashindwa kufanya vema basi atafanya mapinduzi kuwaondoa viongozi hao

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE