July 1, 2017

POLISI IRINGA WABAINI CHANZO CHA AJALI ZA BAJAJI

Kaimu  kamanda  wa  polisi  wa  mkoa  wa  Iringa  John  Kauga  akionyesha  siti feki  ambazo  madereva  bajaji  wamekuwa  wakizifunga mbele  kwenye  siti  ya dereva ili  kuweza  kupakia  abiria  wengi  zaidi 
Siti  feki  zilizotolewa  kwenye  Bajaji  hizi  hapa
Hii  ndio  siti  feki  iliyoongezwa  kwenye  bajaji

JESHI  la  polisi  mkoa  wa  Iringa kikosi  cha  usalama  barabarani  limeanza  msako mkali  wa  kunusuru  wananchi na ajali  za  bajaji  kuwa  kuzikamata  Bajaji  zote  zilizoongeza  siti  ya  feki  mbele  kwenye  usukani wa  dereva  ili  kubeba  abiria  wengi  zaidi.

Kaimu kamanda  wa  polisi  mkoa wa Iringa  John Kauga  alisema katika  msako  huo  unaoendelea  tayari  wamekamata  Bajaji  zaidi ya 12  ambazo  zimeongezwa siti  katika  usukani wa  dereva na  wahusika  kuchukuliwa  hatua  za  kutozwa  faini .

Kwani  alisema  kinachofanywa na madereva  bajaji  hao  kwa  kuongeza  siti hizo ni chanzo  kikubwa  cha ajali kutokana na Bajaji  hiyo  kukosa balance pindi  itakapoongezwa siti  hiyo mbele  kwa  dereva kwa  kulazimisha  kubeba  abiria  wawili  mbili na pamoja na dereva  kuwa na jumla ya   watu  watatu mbele na  siti ya  nyumba  kuwa na watu watatu  ama  zaidi .

Alisema  kimsingi  Bajaji  imetengenezwa maalum  siti ya  nyuma  kubeba  watu  watatu na  mbele  ni dereva  pekee  na  sio  zaidi ya  hapo  .

" Tumeanza  msako  huo  wa  kukamata  Bajaji  zote  zinazozidisha  abiria  kwa  kuwa na  siti  feki  ambazo  zimetengenezwa  kwa mbao kinyume na utaratibu "

Hata  hivyo  alitaka  wananchi  kutokubali  kupanda  Bajaji ambayo  itakuwa  imeongezwa  siti  feki  kwani ni  hatari kwa  usalama  wao  ni ni rahisi  zaidi  kupata  ajali na  kuwa  utambuzi  kuwa  Bajaji  hiyo ina siti  feki  inayoweza  sababisha  ajali ni  pale  unapoona  dereva anapanga  abiria  wawili katika usukani  wake  kwa  kutaka mmoja akae  kulia na mwingine  kushoto na  yeye  kuwa katikati  kuwa  Bajaji  hiyo  ni hatari kwa  usalama  wako.0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE