July 17, 2017

MWALIMU AFUMWA AKIFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI

Mwalimu Abasi Hussein wa shule ya msingi Mwabomba iliyopo tarafa ya Ngula wilayani Kwimba mkoani Mwanza anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kukutwa darasani akifanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha nne mwenye umri wa miaka 17. 
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo mkoani humo na kusema mpaka sasa mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 27 anashikiliwa na jeshi la polisi muda wowote upelelezi ukikamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.
"Babu wa mwanafunzi alipoona mjukuu wake amechelewa kurudi nyumbani alianza kufanya msako alikwenda kwenye shule ya sekondari lakini hakumuona ikabidi aendelee kumtafuta mjukuu wake, ilipofika kwenye muda wa saa sita na kitu alikwenda kwenye shule ya msingi ya Mabomba katika moja ya darasa wakakuta huyo mwanafunzi wa kike akifanya mapenzi na mwalimu mwalimu wa shule hiyo ya msingi ya Mwabomba" alisema RPC Msangi 
Msangi aliendelea kuelezea jinsi babu alivyoweza kuwakamata watu hao
"Yule babu alikuwa ameongozana na watu wengine hivyo walipowaona waliwakamata wakaita na watu wengine, baadaye taarifa zilifika kituo cha polisi na polisi walikwenda na kuwakuta watuhumiwa hao kwenye lile darasa hivyo wakawachukua na kuwafikisha kituoni, hivyo mtuhumiwa yupo kituo cha polisi tunaendelea na mahojiano na taratibu nyingine za kiupelelezi zinaendelea ili tuweze kukamilisha upelelezi tuweze kumfikisha mahakamani kujibu tuhuma hizo" alisisitiza Msangi 
Mbali na hilo Kamanda Msangi ametoa onyo kwa watu wanaojihusisha na mapenzi na watoto chini ya miaka 17 na kusema huenda awe amekubali mwenyewe hilo ni kosa la ubakaji hivyo amewataka kuacha na kusema kufanya vitendo hivyo ni sawa na kuhitaji kwenda jela miaka 30.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE