July 31, 2017

MKAKATI MPYA WA CHADEMA KATIKA KUPAMBANA NA SERIKALI YA MAGUFULI

Kamati Kuu ya CHADEMA   imekutana kwa siku mbili, tarehe 29-30 Julai, 2017 katika Hotel ya Double Tree, jijini Dar es Salaam kujadili hali ya siasa nchini pamoja na ukandamizwaji wa demokrasia .
Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema inasema kwamba katika mambo ambayo Kamati Kuu imejadili ni pamoja na kamata kamata inayoendelea kufanywa na vyombo vya dola dhidi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA maeneo mbalimbali nchi nzima. 
Hata hivyo kikao hicho kimejadili na kufikia maadhimio na hatua za kuchukua katika ajenda ni pamoja na  kuporomoka kwa uchumi na hali ngumu ya maisha kwa watanzania, ambapo  taarifa kamili juu ya maadhimio hayo na hatua zitakazochukuliwa na chama itatolewa kesho Jumatatu tarehe 31 Julai 2017, kwenye kikao na waandishi wa habari kitakachofanyika jijini Dar es salaam.
 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE