July 24, 2017

MESSI AFUTA PICHA ZA NEYMAR KWENYE ISTAGRAM YAKE

Hali bado ni ya sintofahamu katika klabu ya Barcelona kuhusiana na taarifa za mshambuliaji wa Kibrazil Neymar Dos Santos kwani kila kukicha kunaibuka habari mpya.
Jana kulikuwa na habari zinazosema Neymar ameshaanza kuaga marafiki zake Hispania na kuwaambia anakwenda Ufaransa kujiunga na klabu ya PSG.
Hii leo kumeibuka jambo jipya na la kushtusha ambapo mshambuliaji tegemezi wa klabu ya Barcelona Lioneil Messi ameamua kufuta picha za Neymar katika ukurasa wake wa Instagram.
Wapenzi wa Messi wanaomfollow katika ukurasa wake wa Insta waliona picha za Messi zikipungua na walipofuatilia waligundua picha zilizofutwa ni zile Messi alizopiga na Neymar.
Hii inaweza kuwa dalili mpya kuwa wawili hao mwisho wao wa kucheza pamoja umekaribia na pia mwisho wa Neymar kucheza pembeni ya Messi ndio umekaribia.
Taarifa zinasema Neymar amechoka kuwa chini ya Messi na anaona ni bora aende PSG ambako anaweza kuwa mfalme pekee katika klabu hiyo huku pia dau la zaidi ya £200m likiwa na ushawishi mkubwa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE