July 28, 2017

MASHINDANO YA VENANCE MWAMOTO CUP 2017 ,TIMU ZAPEWA VIFAA VYA MICHEZO


Mbunge wa Jimbo la kilolo Venance Mwamoto kulia akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu za tarafa ya Mazombe leo 
MAANDALIZI ya mashindano ya mbunge wa jimbo la  Kilolo Venance Mwamoto Cup 2017 yameanza kwa kasi kwa mbunge huyo kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu zote shiriki .

Akikabidhi vifaa hivyo jioni ya leo katika mji Mdogo wa Ilula Mbunge Mwamoto alisema kuwa jezi kwa ajili ya mshindi ngazi ya kijiji na mpira kwa kila timu shiriki katika tarafa ya Mazombe. 

Alisema kuwa jumla ya timu 120 zinashiriki katika mashindano hayo ya Venance Mwamoto Cup 2017 .

Akielezea juu ya zawadi alisema mshindi wa kwanza atazawadiwa kombe kubwa pamoja na pikipiki kwa ngazi ya wilaya. 

Pia alisema zawadi kwa mshindi wa pili na watatu na zawadi nyingine zitatangazwa baadae kwani wadhamini Wengi wanaweza kujitokeza kudhamini mashindano hayo makubwa kwa wilaya ya Kilolo. 

kwani alisema kusudi kubwa la mashindano hayo ni kuunda timu ya wilaya ya Kilolo na kuwa tayari amefanya mazungumzo na Julio Kiwere na makocha wengine kwa ajili ya kuja kuunda timu ya wilaya.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE