July 21, 2017

MAPACHA WALIOUNGANA WAMEILETEA HESHIMA KILOLO - DC ASIA ABDALAH

Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Asia Juma Abdalah  akiwa na mapacha  walioungana kiwili  wili Maria na Consolata .
 
.................................................................
MKUU  wa wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah anasema mapaja  yatima  walioungana  kiwiliwili  Maria  na  Consolata Mwakikuti (19)  wazaliwa Kijiji  cha Ikonda  wilayani Makete  mkoa  wa Njombe  ambao wamefanya   vizuri  mtihani  wa taifa  wa  kidato  cha sita  kwa kupata  daraja  la  pili wameipa  heshima kubwa  wilaya ya Kilolo na  mkoa  wa Iringa  kwa kuonyesha  wilaya  yetu ya  Kilolo na  Taifa  la Tanzania  chini ya Rais Dkt John Magufuli lilivyoushangaza  ulimwengu katika  sekta ya elimu  Mwandishi  wa makala  haya  Francis Godwin anaandika .
 
Asia anato wito  kwa  jamii   kuchukulia ufaulu  huo kama  sehemu ya somo kwao na kuacha kuwaficha watoto  wenye  ulemavu kwani nao ni  watoto kama  wengine na wanauwezo  sawa na  watoto  wasio na ulemavu .
 
Mkuu  wa shule ya  sekondari  Udzungwa Edward Fue anasema kuwa mapacha  hao  kufaulu  kwao  ni  heshima kubwa kwa shule hiyo na  ni  kielelezo  tosha  kuwa walimu  wapo  kwa ajili ya  kuona elimu  inaendelea  kuwa  bora  na yenye  kumkomboa  mtoto  na  si vinginevyo .
 
Anasema  Maria  na  Consolata walijiunga shule  hiyo  wakitokea sekondari ya Maria na  Consolata mwaka  2016 na  kuwa  kidato  cha tano na  sita  katika  shule  ya  Udzungwa kilianza  mwaka 2015 kwa maagizo ya  serikali ya  kila  shule ya tarafa  kuwa  na kidato cha  tano na  sita  hivyo Mapacha  hao  walivyofaulu na  kutakiwa  kujiunga shule  hiyo kulikuwa na Compinesheni  mbili  pekee  ya  CBG na HGL ila  kutokana na uhitaji wao maalum  walilazimika kuanzisha cominesheni  ya tatu  ambayo wao  walisomea ya  HKL .
 
“ Wao  ni mzao  wa pili  toka  shule  yetu ilipoanzisha kidato cha tano na sita na  kwa  compinesheni  yao wao ni  wa kwanza na  wa mwisho maana  wamefanya vizuri na sasa shule  imefuta compinesheni  waliyokuwa wakichukua mapacha hao na kurudi kama awali  kwa  kuwa na compinesheni mbili  pekee za CBG na HGL na tumefuta ile ya  akina  Maria na Consolata  kutokana na uhaba  wa vyumba vya madarasa na mabweni “
 
Fue  anasema  kuwa pamoja na kuwa  kwa  upande wake na walimu wenzake  hawajashangazwa sana na matokeo  hayo  ila  wameona ni matokeo ya kawaida kwao hasa  ukizingatia  kuwa mbali ya Maria  na Consolata  ni mapacha walioungana  ila  uwezo  wao  ulikuwa sawa na  wanafunzi  wengine ndio maana  wakati mwingine walikuwa wakishindwa katika  mitihani kwa  kushika nafasi  za chini .
 
Mlezi wa yatima hao Fransca Mlangwa (22) mkazi wa Mawambala Kilolo alisema kufaulu kwa yatima hao walishajitabilia kabla ya mitihani na walishasema watapata daraja la pili  katika mtihani huo wa kidato cha sita na  siku  zote  walikuwa  wakitoka  shule kabla ya  kujisomea  walikuwa wakimwomba Mungu na baada ya  hapo  walikuwa  wakifurahi kuwa   wanaona  Mungu anavyozidi  kujibu maombi yao .
 
Mwakilishi wa  kituo  cha  Nyota  ya  asubuhi  ambako mapacha  hao wanaishi Sir Anyesi Mahoro ambae anafanya kazi  kituoni  hapo na Sekondari  ya Maria Consolata anasema  amefurahishwa  sana na matokeo  ya  mapacha  hao  na  wamefuta  dhana  potofu  ya  baadhi ya jamii  ambayo imekuwa  ikiwachukuliwa  walemavu  kuwa hawawezi  chochote .
 
Anasema anatamani  kuona  wanakwenda  chuo kikuu ambacho  ni rafiki  zaidi  kwao   kutokana  na aina ya  ulemavu  walokuwa  nao wanahitaji mazingira  tofauti  zaidi ambayo wataweza kuyamudu kwa kuingia  darasani na  kutoka ,kwani  kwa  uzoefu  Maria  na Consolata walizoea kusoma pamoja  na wenzao  na hata  baada ya kuachana na  wenzao  darasani  walipenda  kujisomea  wenyewe .
 
 Kwa  sasa  wanavyotaraji  kujiunga na chuo  kikuu wanahitaji kujisomea  zaidi na  kuwa na muda  mwingi  wa kujifunza na  wenzao na  kuwa mazingira waliyosoma kidato cha  kwanza  hadi  nne  ya sekondari ya Maria  Consolata  na  yale waliyosoma  kutoka  kidato cha tano  na  sita  ya sekondari  ya  Udzungwa ni mazingira rafiki zaidi hivyo ilikuwa  rahisi  kwao kujifunza bila  tatizo kutokana na wanafunzi hadi  walimu kuwa  marafiki  kwao.
 
Pia  anasema  watoto hao wanahitaji uangalizi  wa karibu kwa kujifunzia kwa  kupewa  walimu  wa ziada  kwa  ajili yao ,pia wawezeshwe  kupata mawasiliano  ya intarnet kwa  ajili ya kutafuta masomo   mbali mbali ya  kujisomea ila  uzuri  wao  wanayakubali mazingira  yoyote  na  hawapo  tayari  kutengwa ni watu wanaopenda kujichanganya  na  kujiona  ni  sawa na watu wengine .
 
Maria  na Consolata wanasema matokeo  yao  walijua  yatakuwa  hivyo  kwani  katika maisha  yao  wamekuwa  wakimtumaini Mungu  na  kila wakati wamekuwa  wakisema na Mungu kupitia maombi na  hiyo ndio  siri kubwa katika maisha  yao yote na  wataendelea  kuitumia siri  hiyo .
 
Mapacha  hao wamewataka  wanafunzi wenzao waliofanya  mtihani wa  Taifa  wa kidato cha nne kutokata tamaa na matokeo ya mtihani  huo kwani kufeli  kwao ni mapenzi ya Mungu na yawezekana Mungu anamakusudi  yake na hawapaswi kujiingiza katika vitendo viovu bila ya  kumshirikisha Mungu kwa maombi ili  kujua wamepangwa  kutumika katika  eneo gani .
 
"darasani kwetu tulikuwa makundi matatu na jumla yetu tulikuwa 76 ambao si wote wamefanikiwa kufaulu ila tunasema wasikate tamaa kufeli darasani si kufeli maisha ila tumefanikiwa  kufika hapa tulipo kutokana kwa neema ya Mungu , misaada ya watu mbali mbali ikiwemo serikali na hivyo wanaamini watafanya vema chuo kikuu kwa kutegemea wadau hao waliofanikisha kufika hapa leo nyumba hii  tunapoishi ni nyumba tumejengewa na masisita wa Misionari wa consolata ambao baada ya kufaulu darasa la saba na kupangiwa jangwani Dar es salaam waliamua kutujengea nyumba hii kwa kuhofia maisha ya Dar es salaam kuwa ya joto.... Ila serikali ilitununulia gari letu kwa  ajili ya matumizi yetu "
 
Kuwa  bado  wanaiomba serikali kusaidia kuwajengea nyumba rafiki katika chuo ambacho watakwenda kusoma kwa  kuwa  maisha ya bweni kwao si rafiki na kuwa kwa  sasa  wanahitaji zaidi  kusoma mazingira nje ya  Kilolo kwa  ngazi ya  chuo iliyopo  mbele  yao .
 
“ Mlezi ambaye amekuwa akitulea hatuoni sababu ya kwenda nae chuo kuendelea kutulea kwa  kuwa nae nae anasoma chuo cha ufundi Veta fani ya ufugaji na yupo mwaka wa kwanza hivyo lazima ajitafutie maisha yake na  tunamshukuru kwa msaada  wake  kwenye maisha  yetu hatutamsahau “
 
Mapacha  hao  ambao kwenye familia yao wazazi wote walitangulia mbele za haki na kwa sasa na sasa wapo watano na kati yao kaka yao na dada walifika chuo kikuu na wanaajira zao mmoja yupo Zambia na mwigine yupo Dar es Salaam huku mdogo wao ataanza kidato cha kwanza mwakani na  kudai  kuwa mara  baada ya  kumaliza chuo wanategemea  kufanya kazi ya ualimu ili  kulipa fadhila kwa  walimu na wote  waliowasaidia kwa kwenda  kufundisha shule .

Wanasema  hawajawahi kufeli somo masomo na wamekuwa wakipishana  iwapo  mmoja atashika upili basi mwingine  hushika ukwanza  darasani na wamekuwa wakishindana hivyo  hadi wanahitimu kidato cha sita japo  kuna  wakati  ambao katika maisha  yao  hawatakuja  kusahau  siku  walipofanya vibaya  mtihani wa Mock.

Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza anasema  kuwa  lengo la  mkoa wa Iringa  kuendelea  kufanya  vizuri  zaidi katika matokeo yote ya mitihani kuanza shule   za msingi hadi  sekondari na  kuwa mkoa huo ni mkoa wa  kielimu na  sasa  idadi ya  wazazi kuendelea  kuhamishia  watoto wao  shule za mkoa wa Iringa inazidi kuendelea na hivyo kuwataka  wananchi kuendelea na ujenzi wa vyumba  vya madarasa ,shule za  sekondari na maabara  za masomo  ya Sayansi .
" Nimefarijika  sana  na matokeo  mazuri ya kidato cha sita  katika mkoa wangu  na  moto huu  usizimike tuzidi kumuunga mkono Rais Dkt Magufuli kwa kuendelea  kuhimiza watoto kupenda kujisomea zaidi na walimu  kuacha maandamano kabla ya  kutumia njia  sahihi  kujfikisha malalamiko  yenu"
 
Afisa  elimu  mkoa  wa Iringa Majuto Njanga  anasema  wilaya ya  Kilolo  imeendelea  kujfanya  vizuri  katika matokeo  yake na kuwa kimkoa ni  wilaya ya  kwanza kwa  kuongoza kwa asilimia 99.61 na kwa  upande wa GPA  pia  imeongoza kwa  kuwa na 3.0351 ikifuatiwa na Mji Mafinga  yenye asilimia 99.73 na  GPA 3.2434 ,wakati Manispaa ya Iringa ikishika nafasi ya tatu  kwa  kupata asilimia  99.01,Mufindi imeshika nafasi ya  nne  kwa  kuwa na asilimia 97.37 na GPA 3.2651  na Iringa DC ikishika nafasi ya tano kwa  kupata asilimia 96.63 na katika GPA Iringa DC imeshika nafasi ya nne kwa  kuizidi Manispaa kwa  kupata GPA 3.6052
 
Kuhusu  wanafunzi  waliofeli na idadi yao katika mabano wilaya ya  Kilolo (1), Mji Mafinga (1),Mufindi (13),Iringa DC (44) Manispaa ya Iringa (5)
Waliofaulu  Kilolo (253) Mji Mafinga (374),Mufindi (481),Iringa Dc (1,375) na Manispaa ya  Iringa (501) wanafunzi  wasiofanya mtihani huo kwa  Kilolo hakuna ,Mji Mafinga (2),Mufindi (2),Iringa Dc  (4) na Manispaa ya  Iringa hakuna .
Ufaulu  kwa  mkoa ni asilimia 98.47 wakati mwaka 2016 ilikuwa ni asilimia 97.9 hivyo  mkoa umezidi  kufanya  vizuri  katika  ufaulu .
Anasema  kutokana na nafasi  kwa GPA shule ya  kwanza na wilaya  yake katika mabano  ni Pomerini  (kilolo) iliongoza ikifuatiwa na Kawawa (mji Mafinga) nafasi ya  tatu Malangali( Mufindi),Ilula , (kilolo),Ismila (Iringa DC) ,Mwembetogwa ( manispaa ya  Iringa ) Kiwere (Iringa DC) , Nyerere Migoli (Iringa DC) ,Changarawe (mji Mafinga ) Igowole (Mufindi) Image ( Kilolo) Mafinga Seminary (Mji Mafinga) ,Consolata Seminary (mji Mafinga) JJ Mungai (mji Mafinga), Udzungwa (kilolo) Tosamaganga (Iringa Dc) , Iringa Girls (Manispaa ya Iringa ), Ifunda Girls (Iringa DC ) Mtera ( Iringa DC ) Lugalo (manispaa ya  Iringa(  Highlands (manispaa ya  Iringa), Sadani ( Mufindi), Ifunda Technical ( Iringa Dc) Medo Mafinga ( mji Mafinga ) na ya 25 ni Efatha (iringa mjini)
 
Hata   hivyo anasema hata  mwaka jana  2016 kiasilimia  wilaya ya  Kilolo iliongoza  katika ufaulu  kwa  kuwa na asilimia 100,Mji Mafinga asilimia 99.7, Mufindi asilimia 99.3, Manispaa ya  Iringa asilimia 97.4 na Iringa Dc asilimia 96.7
https://ssl.gstatic.com/ui/v1/icons/mail/images/cleardot.gif
Baadhi ya  wadau  wa elimu  mkoani Iringa  Julia Sanga  ambae ni  mwalimu mstaafu anasema   kuwa shule  zilizofanya  vibaya  nyingi ni zile za masomo ya  Sayansi na  sababu  kubwa ni kukosekana kwa maabara  za  masomo ya  sayansi zenye  vitendea kazi.
 
Kuwa   vifaa vya sayansi zilikuwa  zikinunuliwa wakati wa mitihani hivyo kuonekana  kuwa  vigeni kwa  wanafunzi hao  ila  shule  Art ndizo zilizofanya  vizuri  zaidi japo  ameishukuru  serikali kwa  mwaka  huu  imenunua  vifaa vya kutosha katika maabara za  sayansi  na upo uwezekano wa matokeo  kuwa mazuri  zaidi ya  hayo
 
 piga  simu yetu  0754026299 kwa  maoni  usikose makala  hii inaendelea   Jumapili ...........

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE