July 19, 2017

MAPACHA WALIOUNGANA IRINGA WAPEWA ZAWADI NA VIONGOZI WILAYA YA KILOLO

SERIKALI  ya  wilaya ya  Kilolo  na mbunge wa  kilolo Venance  Mwamoto wamewapongeza  kwa zawadi  za maandalizi ya chuo kikuu mapacha Maria  na  Consolata  Mwakikuti (19) waliofanya  vizuri  katika matokeo ya  mtihani wa  kidato cha  sita mwaka huu.
Wakikabidhi    zawadi hizo  kwa  mapacha  hao  jana  mbele ya walezi  wao wa kituo  cha Nyota ya asubuhi  ambako wanaishi  Maria  na Consolata  , mkuu  wa  wilaya  ya Kilolo Asia Abdalah  ,mbunge Mwamoto  ambao  waliongozana na mkurugenzi  mtendaji wa halmashauri ya  Kilolo Alloyce Kwezi na mwenyekiti wa CCM wilaya ya  Kilolo  Seth  Moto walisema  wamevutiwa na ufaulu  wa mapata  ambao ni yatima hivyo  wamelazimika  kuwaanzishia maandalizi ya  chuo mapema  zaidi kwa  lengo la  kuwawezesha  kuanza  chuo kwa  wakati .
Mkurugenzi  mtendaji wa Halmashauri ya  Kilolo Kwezi  alisema kwa  kufanya kwao  vizuri  kumeongeza  heshima  kubwa  kwa  wilaya ya  Kilolo ambayo  ndio  iliyoongozwa kwa matokeo ya kidato  cha  sita kwa  mkoa  wa Iringa  wenye  shule 25   huku wilaya   hiyo ikiongoza  kimkoa kwa  kuwa na shule ya kwanza ya  Pomerini  iliyoziongoza  shule  zote 25.
Hivyo  alisema moja kati ya mkakati  wa  Halmashauri ya  Kilolo ni  kuendelea  kufanya  vizuri  zaidi katika mitihani  mbali mbali  pamoja na mambo  mengine ya  kimaendeleo ili  kuifanya  wilaya   hiyo kuwa  mbele kwa  kila jambo .
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia  alisema  kuwa pamoja na wilaya  kutoa  msaada  huo  kwa  watoto  hao mapacha kama  sehemu  yao ya maandalizi ya  chuo bado milango ipo  wazi kwa  wadau  wengine  walioguswa na  watoto hao  kuzidi  kuwasaidia kwani wao  wenyewe  wameonyesha nia ya  kuendelea  na masomo  na  kuwa mfano kwa baadhi ya   jamii ambayo  imekuwa  ikiwaficha  watoto  wenye  ulemavu kwenda  shule .
“ Wametowezesha  wilaya yetu  kufanya vizuri  kweli  tunawapongeza  wao  ,walimu na wadau  wote  wa  elimu  zaidi  wanafunzi  ambao  wamefanya  vizuri katika  mitihani  hiyo  Kilolo ilikuwa ikitazamwa  sana  kuona  nini matokeo ya  watoto hao  Maria na Consolata  ila bila viongozi na  wadau  wengine  wa  elimu  kujitoa kwa  ajili yao yawezekana wasingefanya  vizuri …..tupo pamoja nao na  tutaendelea  kuwa pamoja zaidi hadi  chuo “
Mkuu  huyo wa wilaya  alisema  moja kati ya mahitaji  yao  makubwa  kwa  sasa ni nyumba  yao  maalum kwa  ajili ya kuishi  pindi  watakapokuwa chuo kwani  wao wanahitaji nyumba maalum ambayo ni rafiki zaidi na aina ya ulemavu  waliokuwa nao .
Mbunge  wa  Kilolo Mwamoto  mbali ya kuwapongeza mapacha hao  bado  alitaka  wananchi  wote  wenye  watoto  wenye  ulemavu kuiga mfano wa mapacha hao na hatapendezwa  kuona  watoto  wenye  ulemavu wa aina yeyote  ile  wanafichwa  majumbani .
Pia  alisema moja kati ya mkakati  wake kuona mazingira  ya  shule  mbali  mbali katika  wilaya ya  Kilolo yanakuwa rafiki na  kuwataka  wananchi  kuendelea  na ujenzi wa vyumba vya madarasa  ,maabara  ili  kuepukana na changamoto ya miundo  mbinu ya  elimu  pamoja na kwenda  sawa na serikali ya Rais Dkt John Magufuli ya  uboreshaji wa  elimu .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE