July 18, 2017

MAPACHA WALIOFANYA VIZURI MTIHANI WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2017 WATOA UJUMBE MZITO........


Mapacha  walioungana ambao wamefanya vizuri  katika matokeo ya  kidato  cha  sita  mwaka 2017 Maria  na Consolata Mwakikuti (19)  wakiwa  katika mahojiano  maalum  na mmilikiwa  wa  mtandao wa matukiodaimaBlog Francis Godwin mzee wa matukiodaima jana nyumbani  kwao kituo cha  nyota ya  Asubuhi  Kilolo
Shule  waliyosoma Mapacha hao
........................................................................................................................................................
Na matukiodaimaBlog
YATIMA walioungana kiwiliwili ambao walifanya mtihani wa kidato cha sita na kufaulu kwa kupata daraja la pili Consolata na Mariam Mwakikute (19) wamesema wamefaulu vizuri kwa kumtanguliza Mungu katika masomo yao  
Wadai kuwa muda wote walikuwa wakimtegemea Mungu na ufaulu huo walishasema na Mungu kabla ya mtihani hivyo hawakuwa na wasiwasi wa kufeli.
 
Wakizungumza katika mahojiano maalum namtandao wa  matukiodaimaBlog  kijijini Udzungwa wilaya ya kilolo mkoa wa Iringa wanakoishi katika kituo cha nyota ya asubuhi kilichopo chini ya masisita wamisionary waconsolata yatima hao walisema kuwa ndoto yao ni kuendelea kufanya vizuri chuo kikuu.
 
Huku wakiwataka mabinti wenzao waliofeli kwa kupata alama 0 katika mtihani huo wa kidato cha sita kutojutia wala kujiingiza katika ukahaba ama mambo yasiyofaa zaidi ya kuendelea  kumwomba Mungu ili awaonyeshe vipaji vyao.
"darasani kwetu tulikuwa makundi matatu na jumla yetu tulikuwa 76 ambao si wote wamefanikiwa kufaulu ila tunasema wasikate tamaa kufeli darasani si kufeli maisha "
 
Yatima hao walisema wamefanikiwa kufika hapa walipo kutokana na misaada ya watu mbali mbali ikiwemo serikali na hivyo wanaamini watafanya vema chuo kikuu kwa wao kuendelea kumtanguliza Mungu na kwa  misaada ya  wadau hao waliofanikisha kufika hapa leo.
 
"Hapa tunapoishi ni nyumba ambayo tumejengewa na masisita wa Misionari wa consolata ambao baada ya kufaulu darasa la saba na kupangiwa jangwani Dar es salaam waliamua kutujengea nyumba hii kwa kuhofia maisha ya Dar es salaam kuwa ya joto Ila serikali ilitununulia gari letu "
 
Walisema wanaomba serikali kusaidia kuwajengea nyumba rafiki katika chuo ambacho watakwenda kusoma maana maisha ya bweni kwao si rafiki.
 
Kuhusu mlezi ambaye amekuwa akiwalea walisema hawaoni sababu ya kwenda nae chuo kuendelea kuwalea maana nae anasoma chuo cha ufundi Veta fani ya ufugaji na yupo mwaka wa kwanza hivyo lazima ajitafutie maisha yake.
 
Aidha walisema wao kwenye familia yao wazazi wote walitangulia mbele za haki na kwa sasa  wapo watano na kati yao kaka yao na dada walifika chuo kikuu na wame ajira  kaka yao yupo nchini  Zambia na mwigine yupo Dar es Salaam huku mdogo wao ataanza kidato cha kwanza mwakani.
 
Mlezi wa yatima hao Fransca Mlangwa (22) mkazi wa Mawambala Kilolo alisema kufa
ulu kwa yatima hao walishajua mapema  kabla ya mitihani na walishasema watapata daraja la pili  katika mtihani huo wa kidato cha sita.
 
Alisema wakati wote walikuwa wakitenga muda wa masaa mawili ya kumwomba  Mungu na kusoma na baada ya hapo walikuwa wakimshukuru Mungu kabla ya kulala na  wanapoamuka
Mkuu wa shule ya sekondari ya Udzungwa Edward Fue alisema kuwa kufaulu kwa yatima hao mapacha kumepokelewa kwa shangwe na dunia nzima kutokana na wengi kupiga simu kupongeza.
 
Kuwa wengi walikuwa wakipiga simu si tu kujua shule imeshika nafasi ya ngapi ila walitaka kujua Maria na Consolata kama wamefaulu.
 
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Asia Juma Abdalah anasema  kuwa  kilichofanywa na mapacha  hao  ni  kutokana na kazi  nzuri ya  serikali ya  awamu ya  tano  chini ya Rais Dkt  John Magufuli na  kuwa ........
Endelea kufuatilia undani wa  mfulilizo wa Makala  haya  ndani ya magazeti ya Mtanzania  na Rai pia katika mtadao huu  Pia usikose Video ya mahojiano haya
Piga simu 0754026299

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE