July 18, 2017

MAKAMU WA RAIS KUZUNGUMZIA UTAWALA BORA NCHINI

Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, kesho Julai 19, 2017 jijini Dar es Salaam, anatarajiwa kuzindua ripoti ya kwanza ya utawala bora nchini, iliyoandaliwa na Taasisi ya Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa Afrika Kujipima kwa Vigezo vya Utawala Bora (APRM), Uliobuniwa na viongozi wa Umoja wa Afrika mwaka 2003.
Akizungumza na Wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa APRM-Tanzania, Dkt. Rehema Twalib amesema ripoti hiyo imebeba maoni ya wananchi kuhusu changamoto na mafanikio ya utawala bora kwenye masuala manne ikiwemo, demokrasia na siasa, uchumi na huduma za jamii.
Amesema lengo la uzinduliwaji wa ripoti hiyo iliyoandaliwa tangu mwaka 2012, ni utekelezaji wa matakwa ya kiutaratibu katika mchakato wa APRM kwa lengo la kuitaka serikali kuanza utekelezaji rasmi wa changamoto za wananchi zilizoandikwa kwenye ripoti hiyo.
“Ripoti hii inaandaliwa kila baada ya miaka minne baada ya changamoto zilizoainishwa kwenye ripoti ya awali kufanyiwa kazi na serikali,” amesema.
Kwa upande wa mmmoja wa wajumbe wa jopo la watu mashughuli wanaosimamia mchakato wa APRM nchini, Rachel Mukamunana, amesema kutokana na juhudi za Rais John Magufuli katika kuhakikisha uwepo wa utawala bora, ana Imani kuwa changamoto zilizopo katika ripoti hiyo zitatuliwa kwenye kipindi cha utawala wake.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE