July 6, 2017

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SADC

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amezitaka Taasisi za Maendeleo ya Fedha za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuimarisha ushirikiano na kubadilisha uzoefu katika utendaji wao wa kazi ili kuhakikisha kazi zinazofanywa na Taasisi hizo zinakuwa na manufaa kwa wananchi wa Jumuiya hiyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua Mkutano wa mwaka wa Taasisi za Maendeleo ya Fedha za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kama taasisi hizo za kifedha zitafanya kazi kwa kuzingatia ubunifu na uaminifu ana uhakika kuwa malengo waliyojiwekeza yatafikiwa kwa wakati hasa katika uwekezaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ameeleza kuwa bado upo umuhimu mkubwa kwa Taasisi hizo za Kifedha katika nchi za SADC kuendelea kutumia ipasavyo wataalamu wa vyuo vikuu na taasisi za utafiti kwa lengo la kukuza uchumi unaotokana na ujuzi kupitia ubunifu.

Makamu wa Rais pia amehimiza nchi wanachama wa SADC kupitia taasisi za kifedha za nchi hizo kushirikiana katika kuchangia fedha katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji amesema anaimani kubwa kuwa mkutano utasaidia kwa kiasi kikubwa uimarishaji wa utendaji wa kazi katika Taasisi hizo za Maendeleo ya Fedha katika nchi za SADC.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE