July 5, 2017

MAKADA NANE CCM IRINGA WAJITOSA KUMRITHI JESCA MSAMBATAVANGU

JUMLA  ya  wanachama 8  wa  chama  cha  mapinduzi (CCM)  mkoa  wa  Iringa wamejitokeza  kuchukua  fomu ya  kuwania nafasi  ya uenyekiti  wa mkoa  nafasi  iliyokuwa  ikiongozwa na Jesca  Msambatavangu  aliyevuliwa  uongozi .
Idadi  ya  wanachama  hao  waliochukua  fomu  imeonekana  ni  kubwa  zaidi  kwa  kipindi  kifupi ya  siku  tatu  toka  zoezi   hilo  lilipoanza Julai 2 mwaka huu ukilinganisha na  nafasi nyingine ambazo  baadhi ya  nafasi hadi  sasa  ina mwanachama  mmoja  pekee  aliyechukua  fomu .
Katibu  wa  CCM  mkoa  wa Iringa Christtopher Magala  aliwaeleza  waandishi wa habari  leo   ofisini  kwake  kuwa   nafasi ya  kiti  mkoa   wanachama  nane  ndio  waliojitokeza  hadi  jumatatu  jioni  wakati nafasi ya ujumbe wa NEC  mkoa  wanachama  watano  wamejitokeza  na nafasi ya  NEC taifa   wamejitokeza  wanachama 6  huku  ukatibu mwenezi  wa  mkoa kajitokeza  mwanachama mmoja  pekee.
Aliwataja  wanachama  ambao  wamejitokeza  kugomea nafasi ya  kiti  mkoa  kuwa ni  Epherehem Mhekwa , Godfrey  Mosha , Daniel Kidava, Listen Mpesa, Yustino Mdesa , Seth Moto , Albath Chalamila na  Joseph Luhwago .
Wakati nafasi ya  ujumbe wa NEC mkoa  waliochukua  fomu  hadi  sasa  ni  Salm Abri , Adestino Mwilinge, Asad Kikunile ,Mahamoud Madenge na Michael Mlowe .
Waliojitokeza  kuchukua  fomu ya  ujumbe wa NEC Taifa  kapu ni Experius Chota , Antpas Mbughuni ,Listen Mpesa , Bernad Mbugu, Azizi  Lisasi  na Antony Mtumbuka .
Katibu  huyo wa CCM mkoa wa Iringa  alisema hadi  sasa  nafasi  ya ukatibu  mwenezi mkoa  fomu  imechukuliwa na  Asad Kikunile  wakati waliochukua  fomu ya ujumbe wa Halmashauri  kuu ya mkoa ni Leah Mwamoto , Ashura Jongo  na  Asad  Kikunile .
Akielezea  kuhusu kasi ya uchukuaji wa  fomu katika  jumuiya  nyingine ndani  ya  chama  hicho  alisema  hadi  sasa  jumuiya ya wazazi wanachama 17 wamechukua  fomu katika  , UWT  wamejitokeza  wanachama 12 na  UVCCM wanachama 25 kwa ngazi ya  mkoa na kwa  wilaya  zote  UVCCM wamechukua  vijana 44.  
Hata  hivyo katibu  huyo  aliwataka  wana CCM  kuendelea  kujitokeza  kuchukua  fomu  za uongozi  na kuwa  fomu  hizo  zinatolewa  bure  bila malipo na  iwapo  mtendaji  yeyote wa CCM mkoa wa Iringa atamtoza  pesa mwanachama  yeyote  atachukuliwa hatua  kali .
Pia  alisema  chama  hakitamvumilia  mwanachama  yeyote  atakayebainika  kufanya kampeni za  kumchafua  mwanachama  mwingine  kwa  njia  yeyote  ile .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE