July 18, 2017

LINAH MWAKYEMBE AGWA LEO DAR ESALAAM


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Samia Suluhu Hasan amewaongoza waombolezaji kuuaga mwili wa mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo marehemu Linah George Mwakyembe katika usharika wa kanisa la KKKT- Kunduchi DSM.
Pamoja na Makamu wa Rais, pia ibada hiyo imehudhuriwa na marais wastaafu mzee, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete pamoja na Mawaziri,  Katibu Mkuu kiongozi, makatibu wakuu na wawakilishi kutoka ofisi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania.
Akizungumza mmoja ya watoto wa Waziri Mwakyembe ambaye amesoma wosia wa marehemu mama yake, Bi Linah amesema mama yake alikuwa ana ngozi ngumu kuliko hata mzee wake na alikuwa akimfariji na kumpa moyo endapo zinapotokea changamoto katika kazi yake.
Waziri wa Habari Dkt Harrison Mwakyembe akilia kwa uchungu juu ya Jeneza la mkewe wake Linah Mwakyembe wakati wa kutoa heshima za mwisho leo.
Marehemu Linah Mwakyembe mzaliwa wa Machame Wari huko Kilmanjaro mwaka 1970 na alifariki dunia tarehe Julai 15 mwaka huu saa tano usiku katika hospitali ya AGA KHAN alipokuwa anauguzwa maradhi ya saratani ya matiti ambayo imemsumbua kwa miaka miwili na ameacha mume na watoto watatu wa kiume. 
Prof Anna Tibaijuka Mbunge wa Muleba Kusini akitoa heshima zake za mwisho.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE