July 19, 2017

KESI YA MANJI YASOGEZWA MBELE BAADA YA KUUGUA GHAFLA


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeahirisha kesi inayomkabili Yusuph Manji, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, anaandika Hamisi Mguta. Manji ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu hapa nchini anakabiliwa na kesi ya kukutwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania pamoja na mihuri kadhaa ya jeshi hilo kinyume cha sheria.
Kesi hiyo iliyopangwa kusikilizwa leo, haikusikilizwa kutokana na mahakama kuambiwa kwamba upelelezi wake haujakamilika.
Aidha, jana mtuhumiwa huyo alikwama kufika mahakamani hapo kwa madai kwamba ni mgonjwa na anadaiwa kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Madai hayo ya Manji kuumwa yametolewa leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na wakili wake.
Kesi ya mfanyabiashara huyo imepangwa kusikilizwa Agost 4, mwaka huu.
Manji alisomewa mashtaka saba Julai 5 mwaka huu akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na watuhumiwa wenzake, kwa makosa ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE