July 29, 2017

JOKETE KUFANYA HAYA LEO JUMAMOSI...

Balozi wa mpira mpira wa kikapu Tanzania, Jokate Mwegelo, kesho anatarajiwa kushuhudia mchezo wa Ligi ya Vijana (U-16), kati ya Don Bosco dhidi ya Msasani, utakaopigwa kwenye Uwanja wa JMK Park, Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Vijana Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Bahati Mgunda, alisema ujio wa Jokate katika mechi za kesho una umuhimu mkubwa hasa katika kuhamasisha wachezaji kucheza kwa viwango.

“Ligi yetu ya vijana itaendelea wikiendi hii ambapo tutakuwa na Balozi wa Kikapu Tanzania anayefahamika kwa jina la Jokate, ambaye pia ni mwigizaji na msanii wa kizazi kipya cha muziki hapa nyumbani.
“Ujio wa Jokate una umuhimu mkubwa hasa katika kuhamasisha timu zinazoshiriki ligi hii kujituma ili bingwa apatikane,” alisema Mgunda.
Mbali na hilo, Mgunda alisema Jokate atapata nafasi ya kuzungumza na wachezaji wa kike wa mchezo huo akiwamo nahodha Jescar Ngisaise, ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuhudhuria mafunzo soma zaidi gazeti la Bingwa jumamosi Julai 28/2017 Ahsante 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE