July 18, 2017

IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO YA JESHI LA POLISI

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro

Dar es Salaam. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko ndani ya jeshi hilo.
Katika mabadiliko hayo, Kamanda Sirro amemteua aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda kuwa Mkuu wa Kitengo cha Mafao na Fidia Makao Makuu ya Polisi.
Taarifa iliyotolewa leo Jumanne, Julai 18 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnaba Mwakalukwa, imeeleza kuwa nafasi ya Kaganda imechukuliwa na Kamishna Murilo Jumanne.
Kabla ya hapo, Kamanda Jumanne alikuwa Kamanda wa Polisi, mkoa wa Shinyanga.
“Nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Jumanne, Shinyanga, imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Simon Sylverius ambaye alikuwa Ofisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Mara,” amesema.
Taarifa hiyo imesema, mabadiliko hayo ni ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Polisi ili kuongeza ufanisi na utendaji wa kazi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE