July 31, 2017

HUYU NDIYE MRITHI WA NIYONZIMA YANGA


Hatimaye kiungo mshambuliaji wa timu ya Taifa Stars na klabu ya Mbeya City Raphael Daud ameingia mkataba wa miaka miwili na Mabingwa wa Kihistoria Yanga ambaye anatajwa kuwa Mbadala wa Haruna Niyonzima ambaye amehamia Simba.
Msimu uliopita akiwa Mbeya City alifunga jumla ya magoli nane na sasa amekamilisha usajili wake rasmi na tayari amejiunga na kambi ya Yanga ambayo ipo mkoani Morogoro na kesho ataanza mazoezi pamoja na mshambulizi Donaldo Ngoma aliyejiunga leo.
Yanga imepiga kambi ya Siku kumi na inatarajia kurejea Agosti 4 na itacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya matajiri wa Singida timu ya Singida United iliyochini ya kocha wa Zamani wa Yanga,Hans Van Der Pluijm na mchezo utachezwa Jumapili kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Agosti 6.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE