July 7, 2017

HIFADHI YA MAZINGIRA YA ASILI KILOMBERO ILINDWE - DC ASIA ABDALAH

Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia  Abdalah  katikati  akiwa na kamati  yake ya  ulinzi na usalama pamoja na mhifadhi  mkuu wa  hifadhi ya mazingira  ya  asili ya  Kilombero Elia Mndeme wa  nne kulia jana  baada ya  kutembelea  hifadhi hiyo eneo la kata ya  Udekwa  wa  pili  kushoto ni  mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya  Kilolo Allocye Kwezi
Dc  Kilolo  akitazama  mazingira  ya  utalii  hifadhi ya  Kilombero
Mkurugenzi  wa  Halmashauri ya  Kilolo Alloyce  Kwezi kushoto  waliokaa akiwa na wadau  wa  utalii  Kilolo  katika  hifadhi ya  mazingira  ya asili ya  Kilombero
Picha ya  pamoja na  wadau  wa utalii  Kilolo
Kamati ya  ulinzi na usalama na  viongozi wa CCM Kilolo
Afisa ufugaji nyuki kanda ya  Udekwa Nuru  Nema Mbwela  akionyesha mizinga  ya  nyuki
Mhifadhi mkuu  wa  hifadhi ya Kilombero Elia Mndeme kushoto  akiiongoza kamati ya  ulinzi na usalama  Kilolo pamoja na  wadau wa utalii  kutembelea  hifadhi  hiyo
Dc  Kilolo  Asia  Abdalah na  mhifadhi  mkuu  Elia Mndeme  wakijadili jambo
Dc  Kilolo  Asia  Abdalah  akizungumza na  wanahabari  baada ya  ziara   hiyo
Wadau  wa utalii kilolo katika  picha ya pamoja na Deo Mwanambilimbi mkurugenzi wa Kalunde  Bendi
Mshauri   wa maliasili  mkoa wa Iringa Alloyce Mawere akitazama  mizinga ndani ya  hifadhi ya mazingira ya asili  Kilombero
 
Na MatukiodaimaBlog
SERIKALI  ya  wilaya ya  Kilolo  mkoani  Iringa  yawataka  wananchi  wanaozunguka  hifadhi ya mazingira  ya asili ya Kilombero wilaya  humu  kuwafichua wageni  wawasioeleweka  wanaofika  kijiji kwao kwa  lengo la  kufanya  ujangili  pamoja na   wananchi wenzao   wanaoshirikiana na majangili  wakiwemo wale wanaochoma moto ovyo maeneo  yanayozunguka  hifadhi  hiyo .
 Rai   hiyo  imetolewa jana na  mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah   wakati  wa  ziara  yake  na kamati ya  ulinzi  na usalama  katika  hifadhi   hiyo ya mazingira  ya  asili  ya  Kilombero  kwenye  kata  ya  Udekwa  wilayani  humo kwa  lengo la  kuhamasisha  utalii  wa  ndani  kwa wananchi wa  wilaya  hiyo na  nje ya  wilaya  hiyo.
Alisema  kuwa   ili  kuwezesha  hifadhi  hiyo  kuendelea  kuwavutia  watalii  zaidi  na  wawekezaji  kufika  kujenga hoteli  za  kitalii ni  vema  suala la  uhifadhi linalofanywa  na  wasimamizi wa hifadhi  hiyo  likawa  endelevu kwa  jamii  inayozunguka hifadhi  hiyo  ili kuhakikisha  wanalinda  hifadhi  hiyo na  kuwafichua wenzao  wanaojishughulisha na  vitendo  vya  ujangili wa  wanyama  ndani  ama  nje ya  hifadhi  hiyo.
“ Kamati  yangu  ya  ulinzi na  usalama  wilaya  ya  Kilolo itaendelea  kupita katika  vijiji  vyote  vinavyo  zunguka   hifadhi  hii  na  kuwachukulia  hatua  kali  wananchi ambao  wanawahifadhi  wageni  ambao  si  wema  wenye  lengo la  kushirikiana na  wananchi kufanya  ujangili kwenye hifadhi …..lazima  wananchi  kutowafumbia  macho wageni wenye  nia mbaya katika maeneo  yetu”
Mkuu  huyo  wa  wilaya  alisema  kuwa  katika  kuendelea  kuhamasisha  utalii  wa  ndani wilaya  hiyo  imejipanga  kuona  vivutio  vyote vya  utalii  vinatambuliwa  ili  kuweza  kuwavuta  watalii  wa  ndani na nje  na hata  wawekezaji kufika  kuwekeza katika  sekta ya utalii ambayo  katika  wilaya ya Kilolo  ina  vivutio vya  utalii  vingi  ambavyo  vinavutia  zaidi  kuliko  hata  vivutio  vya maeneo  mengine  .
Mkurugenzi  mtendaji  wa Halmashauri ya  Kilolo Alloyce  Kwezi alisema  kuwa  wilaya  hiyo  imetenga  maeneo  mbali mbali ya  uwekezaji wa aina  tofauti  tofauti  na  kuwa  wananchi wanaohitaji  kuwekeza wanakaribishwa  kuwekeza  katika  wilaya  hiyo yenye  vivutio  mbali mbali  pamoja na maeneo  mazuri  ya  Kilimo cha  kawaida na umwagiliaji .
Mhifadhi  mkuu  wa hifadhi  ya mazingira ya asili ya  Kilombero Elia  Mndeme  alisema kuwa  hifadhi  hiyo  yenye  ukubwa wa hekta 134,511   ilipandishwa hadhi kuwa  hifadhi ya  mazingira ya  asili Agosti 17 mwaka  2007 na  kutangazwa  katika gazeti la  serikali  namba 182 kuwa   hifadhi  hiyo imetokana na muungano wa  misitu  ya  hifadhi tatu ambayo ni Matundu ,Lyondo na  west Kilombero scarp
Alisema  kiutawala  hifadhi  hiyo  inajumuisha  wilaya mbili  ya  Kilolo  mkoa  wa Iringa na Kilombero  mkoa  wa  Morogoro  na  kuwa  hifadhi   inazungukwa na  vijiji 21 ambavyo  vimegawanyika katika  kanda  kuu  nne kwa  ajili ya  kurahizisha  usimamizi  na kutaja  kanda  hizo  kuwa ni Udekwa , Ukwega, Mpofu  na Namwawala
Akielezea  katika  kukabiliana na ujangili  alisema kuwa  wameanzisha  doria  shirikishi kwa  kuwashirikisha  watumishi  wa wakala  wa huduma  za  misitu (TFS) hifadhi  ya Taifa  ya milima ya Udzungwa (UMNP) kikosi  cha kuzuia ujangili (KDU),askari  mgambo  wa  kijiji (VGS) na kamati  za mazingira  za  vijiji (VNRC’S ) kutokana na mpango  kazi kamati  hizo  kila robo  mwaka  zinapaswa  kufanya  doria  zisizopungua 17.
Usikose  Makala  maalum katika  gazeti la  Rai

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE