July 12, 2017

HAYA NDIO MATUKIO MAKUBWA YA WACHEZAJI WA EVERTON LEO TANZANIA

  Chrispin kisinini ni mhehe wa kwanza kupiga picha Rooney 
Mashabiki wengi wa soka ya England wamesafiri Tanzania kushuhudia Everton wakichuana na mabingwa wa Kenya, Gor Mahia katika uwanja wa taifa wa michezo jijini Dar es Salaam.

Uwanja huo una uwezo wa kutoshea mashabiki 60,000.
Rooney anatarajiwa kucheza katika mechi hiyo ya Alhamisi.

Wengi wa mashabiki waliofika nje ya hoteli wanamokaa Everton jijini Dar es Salaam waliimba "Rooney Rooney" mchezaji huyo aliposhuka kutoka kwenye basi kuingia hotelini.

Kulikuwa pia na kundi la raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao walijawa na furaha kumuona mwenzao Yannick Bolasie.

Waliimba nyimbo za kitamaduni za DR Congo naye Bolasie akawajibu kwa kucheza.

Mechi ya kesho imeandaliwa na kampuni ya SportPesa kusherehekea udhamini wa jezi za klabu ya Everton.

Wakati wa ziara yao, wachezaji wa Everton pia wataandaa vikao vya mafunzo ya soka na kucheza pia dhidi ya timu mseto ya wachezaji wenye matatizo ya ngozi, Albino United, kuhamasisha watu kuhusu mashambulio na dhuluma ambazo zimekuwa zikitendewa watu wenye ulemavu huo.

Wengi wamekuwa wakiuawa Tanzania na nchi jirani kwa sababu ya ushirikina.

Wachezaji hao baadaye wameelekea shule ya watoto wenye ulemavu ya Uhuru Mchanganyiko jijini Dar es Salaam.
Shule hiyo hupokea ufadhili kutoka kwa shirika la kutoa msaada nchi za nje la Uingereza, DFID.
Baadaye, wachezaji hao wanatarajiwa kucheza na watoto hao.
Wachezaji ngoma wa Kimaasai waliofika kuwatumbuiza wachezaji hao
Wachezaji wa Everton wakiwa shule ya Uhuru Mchanganyiko
Wachezaji  wakisalimiana na  wanafunzi wa  shule ya Uhuru Mchanganyiko  leo (picha na BBC)

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE