July 5, 2017

TUPO PAMOJA NA JPM KUONA KILOLO YA UCHUMI WA VIWANDA -DC ASIA

Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah
.............................
WAKATI serikali  ya  awamu ya tano chini ya  Rais Dkt  John Magufuli ikiwa inapanga kuwa nchi yenye uchumi wa viwanda ifikapo 2025, juhudi za serikali kwa sasa ni  kuhamasisha uanzishaji wa viwanda kuanzia vya  kati ,vidogo hadi vikubwa kwa  lengo  la kufanikisha mchakato huu ambao  tayari  baadhi ya  wakuu wa mikoa na  wilaya  nchini wamekwisha  anza  kwa  kasi  kuamasisha utekelezaji  wa  mipango mahususi ya kujenga viwanda vidogo, hasa katika  sekta ya kilimo, ambako malighafi hutokea kwa wingi na rahisi ila  viwanda  huwa  chanzo  cha  wakulima kupoteza  mitaji  yao.

Kupitia sekta  hii ya kilimo inahitaji maboresho na kuongeza nguvu kwa sababu watu  na wananchi wengi wameajiriwa huko na  ni  wazi  kuwa  mipango yakinifu  na ushiriki  mkubwa wa wakuu wa  mikoa  ,wilaya  na  wadau  wa  sekta hiyo unahitajika  zaidi  ili ifikapo  mwaka 2025  kusiwe na maswali  tena ya  utekelezaji wa  mpango  huu  mzuri wa  serikali .

Mkuu  wa  wilaya ya Kilolo  mkoani Iringa  Asia  Abdalah anasema  kuwawilaya ya  Kilolo ambayo ni  moja kati ya  wilaya  ambazo  wananchi  wake  ni  wazalishaji wa nyanya  ,matunda ,vitunguu na miti na mazao  mengine  tayari  imekuwa na mkakati wa  kutomuangusha  Rais Dkt Magufuli  kwa kuanza  kuweka mazingira  rafiki  yenye  kuwavutia  wawekezaji nchini  kuendelea  kuwekeza  ndani ya  wilaya hiyo katika  sekta ya  viwanda .

Wilaya ya  Kilolo  ina  jumla ya hekta 5,649 zinafaa kwa kilimo  cha  umwagiliaji zikiwa  tayari  zimeboreshwa  kwa  kilimo cha  umwangiliaji  hadi  sasa  eneo  linalotumika kwa  kilimo cha  umwagiliaji  ni hekta 1,810  wakati  skimu za  umwagiliaji  zipo 9 zilizoboreshwa na zinazotumika kwa umwagiliaji ni 7 ambazo ni Ruaha  Mbuyuni yenye ukubwa  wa Hekta 256 yenye wanufaika 1,391, Nyanzwa  yenye ukubwa  wa hekta 250 ina wanufaika 1300 ,Mgambelenga  skimu  yenye  ukubwa wa hekta zaidi ya  2000 ipo  mbioni  kukamilika  itanufaisha watu  10,000 kutoka  vijiji  vitatu  vya Mtandika , Ruaha mbuyuni  na Msosa,wakati  Skimu ya  Mgowelo yenye ukubwa wa hekta 190 yenye wanufaika 350

Usikose kujipatia nakala ya gazeti la Rai kwa undani zaidi... 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE