July 25, 2017

DC SIKONGE ATAKA PEMBEJEO ZA KILIMO ZIFIKE KWENYE WILAYA YAKE KWA WAKATI....

Mkuu wa Wilaya Sikonge Peres Magiri akifungua Maafunzo ya Maafisa Ugani.
Baadhi ya afisa ugani wilaya ya sikonge mkoani Tabora wakiwa katika kikao na Dc
................................................
Na Hellen Isdory,Tabora

RAI imetolewa kwa wataalamu wa kilimo wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora kutakiwa kuandaa mashamba mapema na kujua mahitaji yao muhimu katika maadalizi hayo ili kupata pembejeo za kilimo mapema na kwa wakati Muafaka kabla ya Msimu wa kilimo haujaisha.

Mkuu wa wilaya ya Sikonge Peres Magiri wakati akifungua Mafunzo Maalumu ya Maafisa ugani katika wilaya yake yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya sayansi (COSTECH) kupitia Jua la baiteknolojia nchini (OFAB) yenye lengo la kuwakumbusha na kwenda sambamba na kilimo cha kisasa.

“Tunataka kujua mahitaji mapema na kupeleka mahali ambapo yanahusika ambapo ni serikalini tupate pembejeo kwa wakati kwani zinakuja zinachelewa sas zinawasaidia nini wakulima wetu”Alisema Peres.

“Mwaka jana pembejeo za ruzuku zingine tulikataa tu tulisema hatuhitaji ilikuwa nadhani mbegu za mahindi na mpunga tulisema Msimu umeshapita sasa zinakuja za nini lakini kama tutakuwa na maandalizi mapema ili pembejeo zije kwa wakati na wakulima kunufaika na hizo ruzuku naamini”Aliongezea Peres

Aidha kwa Upande mwingine Mheshimiwa Peres aliwataka maafisa hao ugani kuungana na wananchi katika kuwasaidia kuweka chakula cha akiba na cha kutosha ili kuepukana na baa la njaa kwani kwa sasa wakulima hao wamekuwa wakiuza chakula chao huku bado wakiwa hawana ziada ya kutosha.

“Hali ya mvua kwa mwaka huu haikuwa nzuri ila katika wilaya yangu tulipata mvua za kutosha na wakulima wetu wamelima na tunachakula cha kutosha ila kwa kuwa sehemu nyingine hawakupata mvua hivyo nawasihi wakulima kuangalia wasiuze chakula chote bali wawe na akiba ambayo itaweza kuwafikisha hadi katika msimu mwingine wa mavuno”Alisema Peres

Hata hivyo Katibu wa Chama cha Mapinduzi katika Wilaya Hiyo Emanuel Alex alitoa msisitizo kwa Maafisa hao ugani kutumia elimu waliyopata ili kuanza kulima kilimo cha kisasa ambacho kitaweza kuinua pato lao Zaidi.

“Kwa warsha hii na sisi kama viongozi na maafisa waliohudhuria hapa inatakiwa kutoka na mafunzo haya na kwenda kuyafanyia kazi ili kuanza kuzalisha mazao yetu kwa wingi huku tukiwa tunaenda sambamba na kilimo cha kisasa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE