July 27, 2017

DC KASESELA AMSIMAMISHA MTENDAJI WA KIJIJI

Mwakilishi wa mwekezaji wa mashamba ya George Emmanuel akimkabidhi hati ya ardhi 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akitoa tamko 
Wananchi wa kijiji cha Makongati wakiwa ofisini kwa DC Iringa 
MKUU wa wilaya ya Iringa Richard kasesela amemsimamisha kazi kwa muda
wa wiki mbili kuanzia jana afisa mtendaji wa serikali ya kijiji cha
Makongati kata ya Maboga wilaya ya Iringa mkoani Iringa kwa tuhuma mbali
mbali ikiwemo ya kutumiwa na mwekezaji kunyanyasa wananchi pamoja kutafuna
fedha za vyeti vya kuzaliwa kiasi cha shilingi 12000 zilizochangwa
na wananchi
zaidi ya 100.

Mkuu huyo wa wilaya amechukua uamuzi huo jana baada ya wananchi
wanaoishi kijiji hicho cha Mkongati kufanya maandamano kwa kutembea
umbali wa zaidi ya kilometa 35 hadi ofisini kwake mjini Iringa kumlalamikia
mwekezaji kwa madai ya kutaka kuwapokonya ardhi ambayo walikuwa wamepewa
kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo na mwekezaji wa awali ambaye kwa
sasa ni marehemu .

Awali wananchi wa kijiji hicho walimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa
walipewa hekari 600 na mwekezaji wa awali kwa ajili ya shughuli za kilimo
ila baada ya mwekezaji huyo kufariki dunia familia yake imekuwa
ikiwanyanyasa
kwa kuharibu mazao yao pamoja na kuwataka kuondoka kwenye ardhi hiyo
ambayo walipewa kwa ajili ya kuendelea kulima mazao ya chakula .

Walisema kuwa sababu ya wao kufanya maandamano kufika ofisi ya mkuu
wa wilaya ni kutona na wawakilishi wa mwekezaji huyo George Emanuel
kuwatishi wananchi hao maisha na kuendelea kuharibu mazao yao wanayolima
huku akimtumia afisa mtendaji wa kijiji hicho Allocy Mduda kuwanyanyasa
waanchi kwa kumhonga nyumba ya kuishi aliyojengewa ndani ya ardhi ya
mwekezaji huyo na kuhama kwenye nyumba ya serikali ya kijiji .

Kwa upande wake mwakilishi wa mwekezaji huyo Tomeck Hamaza alisema kuwa
ardhi hiyo wanayoitaka ni ardhi inayomilikiwa halali na mwekezaji na ina
hati ambayo inalipiwa hivyo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi hao
mwekezaji huyo aliwapatia ardhi heka 600 kwa ajili ya kuendesha shughuli
za kilimo ila wao wamekuwa wakikodisha ardhi hiyo kwa watu kutoka
mjini Iringa jambo ambalo

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE