July 12, 2017

CCM MKOA WA IRINGA KUWAENGUA WAGOMBEA WALIOANZA KAMPENI

katibu wa CCM mkoa Christopher Magala 
Katibu wa CCM mkoa wa Iringa akizungumza na wanahabari leo 

Na MatukiodaimaBlog
CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimetoa onyo kwa wanachama wake waliochukua fomu kuwania nafasi mbali mbali ambao
wameanza kukiuka kanuni za chama hicho kwa
kuanza kufanya kampeni wilayani kuwa wataondolewa katika orodha ya wagombea au ama kuvuliwa uongozi mara baada ya
kuchaguliwa .

Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Christopher Magala aliyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake kuhusiana na zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu ambalo limefungwa
juzi ,kuwa kuna taarifa za baadhi ya wagombea
kuanza kuzunguka wilayani kuomba kura kwa
wajumbe jambo ambalo ni kinyume na maelekezo ya chama hicho.

“ Tunaendelea kukusanya ushahidi wao ukikamilika
wataenguliwa katika orodha ya wagombea na kama itabainika baada ya kuchaguliwa watatenguliwa nafasi zao …naomba kutoa onyo kali la kwanza na la mwisho kuwa chama kipo
macho tunataka waheshimu magizo ya chama “

Katibu huyo alisema hadi zoezi hilo linafungwa
jumla ya wanachama 115 walichukua fomu
kuomba nafasi mbali mbali katika wilaya ya Iringa mjini kati yao wanachama 7 hawakurejesha fomu
hizo wakati Iringa vijijini walichukua wanachama
69 na wote walirudisha fomu ,kilolo jumla ya
wanachama 61 ndio walichukua fomu kati yao 6
walishindwa kurudisha fomu huku wilaya ya
Mufindi wanachama 331 walichukua fomu na 8
walishindwa kurudisha fomu hizo na kufanya
idadi ya wasiorudisha fomu kufikia 21.

Alisema kwa nafasi ya mkoa nafasi ya kiti
wanachama wote 13 waliochukua fomu waliweza
kurudisha fomu wakati nafasi ya NEC mkoa wanachama waliochukua fomu walikuwa 13 ila
waliorudisha fomu ni 12 ,NEC – Kapu Taifa
waliochukua fomu ni 30 kati yao wanachama
watano hawakurudisha fomu ,Uenezi mkoa
waliochukua fomu ni 14 mmoja hakuweza
kurudisha fomu na ujumbe wa Halmashauri kuu mkoa wanachama 31 walichukua fomu ila
wanachama watatu hawakurudisha fom na
kufanya jumla ya wanachama 10 ambao
walishindwa kurudisha fomu
Magala aliwataja wana CCM waliojitokeza
kugombea nafasi ya uenyekiti mkoa kuwa ni Seth
Moto, Kelvin Robert, Ally Msigwa , Yohanes Kaguo, George Mlawa , Evans Balama, Joseph
Luhwago,Albart Chalamila,Daniel Kidava, Yustino Mdesa, Listen Mpesa, Godfrey Mosha na Ephraem Mhekwa .

Wanachama waliochukua na kurudisha fomu za NEC mkoa ni Salm Abri , Adestino Mwilinge ,Asad Kikunile (hajarudisha) ,Mahamoud Madenge,Michael Mlowe, Mgabe,Kihongosi,Thom Masini,Enock Ugurumu,Evans Balama,Augustino Mahiga(hajarudisha),Godfrey Mgongolwa ,Marcelina Mkini na Obeid Malima.

Wakati wagombea wa nafasi ya ukatibu Mwenezi
mkoa wa Iringa waliochukua fomu na kurudisha
ni Joseph Mgongolwa , John Kiteve, Godfrey
Mosha, Nasho Kayoka ,Andrew Ghemela,Thobias Kikula,Pius Pius Thadeus Tenga, Josia Kifunge,Ally Msigwa, Ibrahim Ngwada, Denis Lupala, Michael Mlowe,Mwinyikheri Baraza na Asadi Kikunile .

Akitangaza waliochukua fomu za uongozi wa
jumuiya alisema kwa nafasi ya kiti UVCCM ngazi ya mkoa ni 21 kati yao wanachama 18 ndio
waliorudisha fomu hizo ,mkutano mkuu Taifa walichukua 8 na waliorudisha ni 6,baraza kuu walichukua 20 waliorudisha ni 15 mkutano mkuu
wa CCM mkoa walichukua 5 na wote walirudisha
fomu ,mkutano mkuu UVCCM Taifa walichukua
wanachama 4 waliorudisha fomu ni wawili
pekee,mwakilishi wa wazazi walichukua 4
waliorudisha 3 ,mwakilishi wa UWT waliochukua ni 3 waliorudisha fomu 2.

Kwa upande wa jumuiya ya wazazi ngazi ya mkoa kiti walichukua 5 na wote walirudisha fomu ,baraza kuu na mkutano mkuu wa CCM Taifa waliochukua 13 waliorudisha 12,baraza kuu la mkoa nafasi tatu waliochukua na kurudisha ni 8 mjumbe wa baraza la mkoa kutoka kila wilaya nafasi moja waliochukua fomu na kurudisha 8, mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM mkoa walichukua 4 waliorudisha 3, mwakilishi wa UVCCM waliochukua na kurudisha ni 3,mwakilishi
wa UWT aliyechukua na kurudisha ni mmoja pekee .

Magala alitaja idadi ya waliochukua fomu za
uongozi UWT mkoa kwa upande wa Kiti ni wanachama 5 ambao wote walirudisha fomu
,baraza kuu na mkutano mkuu wa CCM Taifa waliochukua ni 8 waliorudisha 7,mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM mkoa waliochukua ni 4 ambao wote walirudisha fomu ,baraza la mkoa nafasi mbili kila wilaya waliochukua ni 18 waliorudisha ni 14,mwakilishi wa wazazi waliochukua ni 5 na waliorudisha ni 4 mwakilishi UVCCM waliochukua na kurudisha ni 2 nafasi ya
NEC wanawake waliochukua na kurudisha ni 2.


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE