July 4, 2017

BUNGE LILIVYOPITISHA MISWADA MIWILI


Wabunge wamejadili na kupitisha miswada miwili ya sheria ya mapitio na majadiliano kuhusu masharti hasi katika mikataba ya maliasili za nchi na mswada wa umiliki wa sheria ya mamlaka ya nchi kuhusiana na umiliki wa maliasili kwa mwaka 2017.
Miongoni mwa mambo yaliyomo katika miswada hiyo ni pamoja na ushirikishwaji wa wananchi katika umiliki wa rasilimali za nchi, uzuiaji wa usafirishaji wa rasilimali nje ya nchi kabla ya kuongezwa thamani, mashauri kati ya mwekezaji na serikali kutopelekwa mahakama za nje na badala yake kutafutiwa ufumbuzi katika mahakama za ndani pamoja na wawekezaji kuhifadhi fedha zao katika benki za hapa nchini.
Jambo jingine ni pamoja na kulipa nguvu bunge kupokea taarifa zote za mikataba ili kujiridhisha kama ina maslahi kwa wananchi na endapo itakuwa ndivyo sivyo basi itarudishwa kwa serikali ili kutengenezwa upya.
Kwa upande mwingine kiongozi wa Kambi Rasmi bungeni, Mhe Freeman Mbowe amesema kuwa jambo la kupitisha sheria ya madini ni jambo jema lakini lilikuwa linahitaji muda wa kutosha ili liweze kuwa na tija zaidi. 
                             kiongozi wa Kambi Rasmi bungeni, Mhe Freeman Mbowe
"Jambo hili kimsingi ni jema ila linahitaji maandalizi ya kutosha ili liweze kuwa na tija inayostahili, tumemsikia Waziri mmoja mwandamizi akisema tulete sheria hata bunge lijalo tunaweza kuifanyia mabadiliko yaani tushatangaza kushindwa kwamba tunatunga sheria tukijua kwamba hatujajiandaa vizuri kwa hiyo hata kwenye bunge lijalo tunaweza kufanya marekebisho ya sheria. Wamarekani walitunga katiba yao zaidi ya miaka 200 iliyopita lakini mpaka sasa imefanyiwa marekebisho mara 14 tu, lakini sisi tunatunga sheria mwaka huu tunarekebisha bunge linalofuata, kwa namna sheria hii inavyopitishwa unaweza kuona hata wachangiaji pale bungeni wanafanya utani", alisema Mbowe. 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE