July 7, 2017

BANDA LA MAZIWA YA ASAS DAIRIES LTD IRINGA YAMVUTIA MAKAMU WA RAIS

makamu  wa  rais  Samia Suluhu  Hassan  akisaini  kitabu banda la   maziwa  ya Asas
Meneja Masoko wa ASAS, Jimmy Kiwelu  kulia  akikaribisha  ugeni  wa makamu  wa  Rais  kuoa ubora  wa  maziwa ya  Asas

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Hassan Suluhu akipatiwa maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa ASAS, Jimmy Kiwelu wakati alipotembelea banda hilo katika maonesho ya Sabasaba

Makamu wa Rais akisaini kitabu cha wageni katika banda hilo la ASAS alipotembelea mapema leo

Makamu wa Rais, Mama Samia akiwa ameshika tuzo ya ASAS ambayo walishinda katika masuala ya usindikaji maziwa. Kulia ni Meneka Masoko wa ASAS, Jimmy Kiwelu akiwa ameshika moja ya tuzo zilizoshinda kampuni hiyo.

Makamu wa Rais, Mama Samia akiwa ameshika tuzo ya ASAS ambayo walishinda katika masuala ya usindikaji maziwa.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Hassan Suluhu, leo Julai 6,2017, ametembelea banda la kampuni ya ASAS Dairies ltd ya Iringa  na kujionea bidhaa

mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo zikiwemo zile za usindikaji maziwa ya aina mbalimbali katika mabanda ya Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Awali Meneja wa biashara na matukio wa ASAS,  Jimmy Kiwelu akimpokea Makamu wa Rais Mama Samia, alimweleza kuwa bidhaa wanazozalisha ni za ubora wa hali ya juu ambapo wananchi wamezipokea kwa mikono miwili.

Pia Jimmy Kiwelu amemweleza  Makamu wa Rais Mama Samia, kuwa kampuni yao imeweza kuibuka washindi wa shindano la usindikaji kwa miaka mitano mfululizo huku wakiendelea kutoa bidhaa zenye ubora wa hali juu.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais amewapongeza  kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa kampuni ya ndani kuweza kuwekeza na kuwa na udhalishaji mkubwa kama huo hapa nchini kwani unasaidia kuimalisha mitaji na uchumi wa ndani.

Mama Samia ameweza kutembelea katika banda hilo ikiwemo kusaini kitabu cha wageni pamoja na kujionea bidhaa mbalimbali kutoka ASAS.
Imeandaliwa na Andrew Chale-MO BLOG
 
 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE