July 19, 2017

BAKWATA WAAGIZA KUKAMATWA KWA ANAYEJIITA MTUME

Baraza Kuu la waislaamu Tanzania Bakwata, limetoa wito kwa vyombo vya dola kumchukulia hatua stahiki mtu aliyejitokeza katika Mkoa wa Pwani na kudai yeye ni Mtume.
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Bakwata, Sheikh Hamisi Said Mataka.
Akizungumza kwa niaba ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Ally, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Bakwata, Sheikh Hamisi Said Mataka, amesema, anachodai mtu huyo aliyetajwa kwa jina la Hamza Issa kuwa yeye ni Nabii na kwamba mafundisho hayo hayapo kabisa katika uislamu.
"Kwa mujibu wa maelezo yaliyoenea katika mitandao ya kijamii na ya kutoka Baraza za Masheikh wa Mkoa wa Pwani chini ya kiongozi wake Sheikh na Qadhi wa Mkoa wa Pwani, amedai kuwa yeye ni Nabii Ilyasa kwa maana ya kwamba roho ya Nabii Ilyasa imemuingia yeye Hamza Issa na kwa hiyo yeye wamekuwa Nabii Ilyasa" amesema Mataka.
Pamoja na hayo, Shekh Mataka amesema mafundisho ya uislamu yako wazi kuwa hakuna Mtume mwingine katika uislamu baada ya Mtume Muhammad (S.A.W) na kwamba upatikanaji wa mtu ndani ya uislamu ya kudai kuwa yeye ni Mtume ni kutaka kuamsha hisia kali za waislamu nchini.
"Baraza la Ulamaa linapenda kuwafahamisha waislamu kwamba, yeyote atakayemfuata mpotoshaji huyu atakuwa ametoka ndani ya uislamu" ,amesisitiza Sheikh Mataka.
Kwa upande mwingine,Baraza la Bakwata limetoa wito kwa Masheikh wa Mikoa, Wilaya na viongozi wa Taasisi mbali mbali za Kiislam kutotoa fursa ya aina yoyote kwa huyo anayejiita Nabii ( Hamza Issa), ili kuzuia kuipotosha jamii.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE