July 24, 2017

AJALI IRINGA YAUA WATATU WAKIENDA MSIBANI RUVUMA

Wananchi  na maofisa  wa  polisi  wakitazama ajali ya gari aina ya  RAV4 iliyoua ndugu watatu  akiwemo mke na mme  waliokuwa  wakienda Mbinga Ruvuma katika mazishi leo huku  watatu wakijeruhiwa
Hii ndio  ajali  iliyoua watatu  leo Iringa
Na MatukiodaimaBlog
WATU watatu  ambao  walikuwa wakielekea  mkoani Ruvuma  katika msiba
akiwemo mke   na  mme  pamoja  na  mfanyakazi wa ndani wamefariki  dunia
papo hapo  na  wengine  watatu  kujeruhiwa  vibaya  baada ya gari  ndogo
waliokuwa wakisafiria kwenda msibani kugongana  uso kwa  uso  na  lenye
namba  za usajili T 866 DMC Mitsubishi Canter.

Imeelezwa  kuwa    wanafamilia  hao  waliokuwa  wakisafiri katika gari aina
ya RAV 4 yenye  namba  za usajili T 795 DGD   walikuwa  wakielekea
Mbinga  mkoani Ruvuma kwa  ajili ya  kushiriki  shughuli za mazishi   walipata
ajali  hiyo eneo la  Kisolanza  katika  wilaya  ya  Iringa kwenye
barabara  kuu ya  Dar  es Salaam  - Ruvuma .

Akizungumza na mtandao huu wa matukiodaimaeneo  la tukio  ndugu wa karibu
na marehemu hao Negro Sanga  alisema kuwa alipigiwa  simu majira ya saa 12
asubuhi ya  leo    na ndugu  waliopo  Dar es Salaam wakimtaka  kufika  eneo
la  tukio  ili  kutoa msaada  kwa majeruhi  hao  ambao  walikuwa
wamepata   waliwapigia  simu  kuomba msaada .

" Hawa  ndugu zangu  walikuwa  wakielekea  Mbinga  mkoani Ruvuma kwa  ajili
ya  kushiriki mazishi  na nimeshitushwa  sana baada ya  kupigiwa  simu ya
rafiki yangu kutoka  Dar es Salaam  asubuhi  sana  kuniomba  nifuatilie
ajali  hiyo  kwani walikuwa hawana msaada  kwa  asubuhi  hiyo ndipo
nilipojulisha  polisi ambao  walifika kwa  wakati eneo la  tukio na
kusaidia  kuokoa maisha ya majeruhi watatu "Sanga  alisema kuwa  baada ya  kufika  eneo  hilo la ajali  tayari
wasamaria  wema  walikuwa  wameitoa  miili mitatu ya  marehemu  hao huku
majeruhi  wakiwa  wametolewa kutoka katika  gari   hilo ambalo  baada ya
kugongana na lori  hilo liligeuka  kuelekea  mwelekeo  ambao lilikuwa
likitoka  huku Lori likiwa  limepinduka upande wa  pili wa barabara  .

“ Waliopoteza maisha katika ajali  hii ni mume ambae  alikuwa ndie  dereva
,mke wake  aliyekuwa amekaa siti ya mbele  pamoja na kijana  wao  wa kazi
aliyekuwa siti ya  nyuma kwa  dereva  pamoja na watu  wengine watatu  ambao
walijeruhiwa  vibaya “


Hata  hivyo  Sanga  anasema katika  ajali  hiyo inaonyesha  mmoja
wapo  alikuwa
amesinzia  na  ndio  sababu ya  kugongana  uso kwa uso huku akidai
kuwa  majeruhi
wote  wamekimbizwa katika  Hospitali ya  wilaya ya  Mufindi kwa matibabu  .


Dereva wa lori ambalo liligongana na gari ndogo  hiyo Issa Markus
alisema  kuwa
eneo  hilo  ni eneo  ambalo lina  mteremko kiasi na wakati akimaliza  kushuka
mteremko  huo gafla dereva wa gari ndogo  hiyo  iliyokuwa  ikitokea
mbele  yake
alihama  upande  wake na  kuja  upande wake na alipojaribu  kumkwepa kwa
alirudi upande  wake  kabla ya  kumfuata  tena  na ndipo  walipoishia
kugongana .

“ Inaonyesha  dereva  mwenzangu ambae sasa ni marehemu  alikuwa amesinzia
maana  nimefanya  jitihada  kubwa sana za kumkwepa  ila bado kanifuata  kama
unavyoona lori langu  likiwa  limepinduka hii   yote ni katika  jitihada za
kumkwepa …..mimi na  utingo wangu  tumetoka  salama ila mimi
nimejeruhiwa  kidogo
sikio la kulia”

Kamanda  wa  polisi mkoa wa Iringa  Julius Mjengi ameuthibitishia mtandao  wa matukiodaimablog   kutokeakwa ajali  hiyo na  kuwa ilitokea majira ya saa  10 alfajiri  na
kuwataja  walipoteza maisha katika ajali  hiyo kuwa ni  Anord  Conrad Kapinda (46) mkazi wa
Kigamboni mkoani Dar es Salaam  ,Maimuna Gwangaya (45) na  Joshua  Aidan
ambae ni fundi  selemara  Mbagala jijini Dar es Salaam.

Alisema  majeruhi  wa ajali  hiyo ni  Neema kapinga (26 ) mwanafunzi  wa chuo cha uhasibu Dar es Salaam , Yohana  Fortino  ( 22)  Fortino Kapinga (55)  wamekimbizwa
Hospitali ya  wilaya ya Mufindi kwa matibabu  huku  akiwataka madereva kuacha  kulazimisha
safari  majira ya usiku na pale  ambapo wanahisi kuwa na usingizi  ni
vema  kuegesha gari na kupumzika .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE