July 14, 2017

ACACIA YAKUBALI KUILIPA TANZANIA

ACACIA Mining Limited imekubali kuilipa serikali mrabaha wa asilimia sita (6%) baada ya sheria ya madini kubadilishwa, anaandika Victoria Chance.
Kampuni hiyo inayomiliki makampuni ya uchimbaji wa madini ya ACACIA nchini imekubali kulipa mirabaha hiyo iliyowekwa katika sheria mpya ya madini.
Sheria hiyo mpya imeitaka kampuni hiyo kulipa asilimia sita ya mirabaha ikiwa ni ongezeko la asilimia mbili (2%) moja ikiwa ya usafirishaji kwenda nje.
ACACIA inaendelea kufuatilia matokeo hayo ya sheria mpya katika mwanga wa maendeleo yake mapya ya madini.
Ikumbukwe kuwa sheria hiyo ya madini ilikuwa mswada mnamo mwaka 2010 na imeanza kutekelezwa mwaka huu.
Aidha, ACACIA ilidaiwa kukwepa kodi hapo awali baada ya kamati ya wakaguzi wa serikali kuwasilisha ripoti ya masuala ya madini kwa Rais.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE