June 26, 2017

WAISLAM IRINGA TUNATAKA RAIS MAGUFULI AONGEZEWE MUDA WA KUONGOZA

waumini wa  dini ya  kiislam  Iringa  mfanyabiashara  Arif  Abri akisalimiana na moja  kati ya  waumini  wenzake  leo  baada ya  ibada  ya  idd uwanja  wa  samora
Waumini wa kiislam mkoa wa Iringa wakitawanyika  katika  uwanja  wa  samora  baada ya  ibada
Waumini  wakipata  picha  za pamoja 
Aliyekuwa mwenyekiti  wa  CCM Iringa mjini Abed  Kiponza  kulia  na Arif  Abri wa  pili  wakiwa na  waumini  wengine
waumini wa  kiislam  wakiwa katika picha  za pamoja
....................................................................................................................................

WAUMINI  wa  dini  ya  kiislam  mkoa  wa  Iringa  wamepongeza  kazi nzuri  inayofanywa na Rais  Dkt  John Magufuli  katika kuwatumikia watanzania na  kuomba  katiba ifanyiwe  marekebisho  ili Rais Dkt  Magufuli aendelee  kuongoza  miaka 35  au  zaidi .

Wakiongea kwa  nyakati  tofauti mara  baada ya  sala  ya  Idd  iliyofanyika  uwanja wa  Samora  mjini  Iringa  waislam  hao  sanjari  na  kumpongeza Rais  Dkt  Magufuli  walisema kipindi  cha  miaka  10  kilichopo  kikatiba  hakitoshi  kulifikisha  taifa  kwenye  mafanikio  zaidi.

Himid  Mbata  alisema  kuwa  wanajivunia  kuwa na  rais  mchapakazi  na mzalendo ambaye  hajapata  kutokea  ukiacha  baba  wa  taifa hayati  mwalimu  Julius  Nyerere .

Hivyo  alisema  njia pekee  ya  kulifanya  Taifa  kuendelea  kuwa  lenye  heshima  ni  katiba  kubadilishwa  ili  kuwa na Rais  wa  kipindi kirefu  zaidi  .

Shehk  mkuu wa  mkoa wa Iringa Abubakari  Chalamila  alisema  kuwa  kazi  kubwa inayofanywa na  rais  ni  faraja  na matumaini  mapya  kwa  watanzania na  kuwa kuendelea  kumpinga  rais wetu  ni  kukosa  uzalendo .

Alisema  hakuna mtanzania ambae  haoni  kazi  inayofanywa na  rais  hivyo  jukumu  kwa kila  mmoja ni  kuzidi  kumuombea  zaidi  ili  aliweke  sawa Taifa  ambalo  lilikuwa  limeyumbishwa .

Pia  alieleza  kusikitishwa na mauwaji ya  Kibiti  mkoani Pwani na  kuwa  kuna haja ya  kuzidisha maombi  kukemea  unyama  huo  kwa wananchi  wasio na hatia .

Shekh  huyo  alisema anatamani  kuona  rais anaendelea  kuliongoza  Taifa  hili  ambalo  lilipoteza imani kwa watanzania kutokana na baadhi ya  wachache  kujinufaisha  wenyewe .

Mbunge  wa  viti maalum  mkoa  wa  Iringa Zainabu  Mwamwindi  (CCM)  alisema iwapo  muswada  wa katiba  utakaotaka  rais Magufuli  kuongezewa muda  wa  kuongoza  ukitua bungeni  hata  kesho  utapitishwa kwani  hakuna  mwanasiasa  ambae  yupo  tofauti na  utendaji kazi wa rais .

Mwamwindi  alisema kuwa mataifa  ya  nje  yanaitazama  Tanzania  mpya kutokana na utendaji kazi wa  Rais  na  kuwa  itapendeza  kuona Rais  anaendelea  kuungwa  mkono  na  kuwataka  wapinzani  wasiopenda  kazi nzuri ya  kuliletea taifa  maendeleo kufunga  midomo  na  kuwa  wao  uwezekano  wa  kuiondoa  CCM madarakani  haupo kwa  sasa .

Mwenyekiti  wa  CCM Iringa  mjini  aliyesimamishwa Abed  Kiponza alisema  kuwa bado  watanzania  waliowengi wanaimani na  serikali ya  CCM chini ya  rais  Dkt  Magufuli  hivyo wale  wanaopinga  ni  vema  wapimwe  akili  zao .

Kiponza alisema CCM ndicho  chama   kilichowakomboa  watanzania na  kitabaki kuwa  chama imara chenye  malengo  ya kweli ya  kuwatumikia watanzania  chini yamwenyekiti  wake  Rais  Dkt  Magufuli .

Amani  Mwamwindi  diwani  wa kata ya Mlandege  (CCM)  alisema  kuwa kinachofanywa na rais  Dkt  Magufuli hakijapata  kufanwa na mwingine  na  kuwa kama  kilifanyika  si kwa  kiasi hiki na  kuwa kwa kasi hii  wapinzani hawana  cha  kupinga .

USIKOSE  GAZETI  LA  RAI ALHMIS  HII

 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE