June 11, 2017

Washauri wakuu wa waziri mkuu wa Uingereza wajiuzulu

                              

Nick Timothy and Fiona HillNick Timothy (kulia) na Fiona Hill                
Washauri wawili muhimu wa waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May wamejiuzulu.
Pia kuna ripoti kwamba wanachama wakuu wa chama tawala cha Uingereza, cha Conservative, wametishia kuanza kutafuta kiongozi mpya, endapo washauri hao hawatotolewa kazini.
Mpambe wake, Nick Timothy, alisema anabeba dhamana kwa mchango wake katika kampeni ya chama, lakini alisema bado anaamini manifesto ilikuwa sawa, manifesto ambayo mwanachama mmoja maarufu alisema ni mbaya kabisa katika historia.
Msemaji wa chama amesema, mwenzake Bwana Timothy, Fiona Hill, piya amejiuzulu.
Bibi May anajaribu kuunda serikali ambayo haina wingi wa viti bungeni, kwa kutegemea chama kimoja cha Ireland Kaskazini.
Theresa May
                                     Bibi Theresa May anajaribu kuunda serikali kwa kutegemea chama kimoja cha Ireland Kaskazini.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE