June 22, 2017

WAISLAM MKOA WA IRINGA WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI WASEMA YUPO KATIKA VITA YA KIUCHUMI WATAKA AOMBEWE

Sheikh  wa waislam mkoa  wa Iringa Abubakar Chalamila akizungumza wakati wafutari  ya pamoja 
Mkuu wa wilaya ya  Mufindi Jamhuri  Wiliam akitoa salam  wakati wa hafla ya  futari  ya  pamoja


Na  MatukiodaimaBlog
UTENDAJI kazi wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli umezidi kuwafurahisha watanzania wa kila kada huku sheikh wa dini ya kiislam mkoa wa Iringa Abubakar Chalamila akiwataka watanzania kuzidi kumuombea ili aendelee kupambana na vita kubwa ya uchumi inayofanywa na mafisadi wachache .

" Vita hii ambayo Rais wetu mpendwa anayoifanya ni vita kubwa na ni vita inayowagusa wakubwa na matajiri wakubwa duniani hii ni vita ya kiuchumi kweli tunampongeza kwa kazi hii nzuri “

Akizungumza wakati wa futari ya pamoja iliyoandaliwa na waislam mkoa wa Iringa katika ukumbi wachuo kikuu cha Ruaha (RUCU) ,Sheikh
Chalamila alisema kuwa utendaji kazi wa Rais Dkt Magufuli ni utendaji unaofanana na ule wa baba
wa Taifa hayati mwalimu Julius Nyerere na kuwa kazi kubwa inayopaswa kufanywa na watanzania ni kuendelea kumpa ushirikiano na kumuombea zaidi .

Alisema katika jamii kuna watu wa aina tofauti wapo Mafisadi ,wezi na hata wengine wenye taifa
kama hizo zisizofaa katika jamii ya kitanzania na
kuwa njia pekee ya kuendelea kuwa na viongozi
wenye hofu ya Mungu ni kuongeza muda wa masomo ya dini katika shule za msingi ,sekondari na vyuo vikuu .

“ Tunadhani makosa yalifanyika awali kwa
kutotoa kipaumbele katika maelezi bora ya hofu
ya Mungu kwani chimbuko la ufisadi ,wezi wa
mali za umma na uadilifu usio mzuri miongoni mwa viongozi wa umma ni kutokana na kuuuza
kipaumbele cha hofu ya Mungu na wengi wanafikiri kwao kipaumbele kikubwa kwa mtoto ni
elimu pekee pasipo kumpa Mungu nafasi “

Kuwa bahati nzuri siku zote Rais Dkt Magufuli
akitoa hotuba zake amekuwa akisisitiza sana watanzania kumtanguliza Mungu kwa kila jambo.

“ Taifa letu limebahatika sana kwa sasa kuwa na
rais mwenye hofu ya Mungu na ndio sababu
kubwa ya nchini yetu imeendelea kung’ara zaidi na kufanya mambo yanayovutia watanzania pia
hata viongozi wa nchi nyingine wanatambua kazi
nzuri inayofanywa na Rais wetu “

Hivyo alisema hofu kubwa iliyopo baada ya Rais Dkt Magufuli kumaliza muda wake ni kukosa
kumpata kiongozi wa mfano wake mwenye hofu ya Mungu kwani hakuna maandalizi yanayofanyika ya kumpata kiongozi mwenye hofu ya Mungu
kama yeye.

“ Tunaiomba serikali kupitia wizara ya elimu
kutoa kipaumbele cha kuweka kipambele cha
elimu ya dini kwa kuongeza muda wa vipindi vya dini badala ya ilivyo sasa muda mfupi sana “

Juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Dkt Magufuli
ambaye ameonyesha wazi kuwa yeye ni kiongozi wa kipekee kwani anachoongea amekuwa
akikimananisha na uzuri hata wasaidizi wake
wamekuwa wakifanya kama yeye anavyotaka .

“ Tunachukua nafasi hii kumpongeza Rais Dkt Magufuli pamoja na serikali yake kwa kazi nzuri
ya kuingia katika vita ya kiuchumi kwa ajili ya watanzania na sisi tutaendelea kuwa nyuma yake kwa kumuombea zaidi “

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam ambae alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza pamoja na kuwapongeza waumini wa dini ya kiislam mkoa wa Iringa kwa kutambua
kazi kubwa na nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt Magufuli bado
alisema yote hayo yanafanywa kwa ajili ya
watanzania wote .

Hivyo alisema kazi kubwa kwa viongozi wa dini na watanzania wote ni kuendelea kumpa ushirikiano na kumuombea sana Rais kwa kuwa anafanya yote hayo kwa faida ya watanzania na
sio kwa ajili yake na ndio sababu kila siku
anatamani kuona watanzania wanakuwa maisha
bora na wote wasio na uaminifu wanawajibika kwa mujibu wa sheria.

Mkuu huyo wa wilaya alisema ndani ya kipindi chake kila mmoja ni shahidi kwa kazi kubwa
inayofanywa na Rais na kuwa ni vema kila mmoja kutambua kazi hiyo badala ya kubeza .

Alisema kuwa dira ya Taifa ni kuwa na Taifa la
uchumi wa viwanda ili kuona watanzania
hatuendelei kutegemea misaada kutoka kwa
wahisani ila inakuwa ni nchi ambayo inajiweza .

Kuhusu suala la maadili mema alisema kuwa anaungana na waislam kuona kuwa elimu ya
dini inaendelea kutolewa katika mashuleni kwani
yawezekana elimu ya dini inayotolewa sasa ya
mara moja kwa wiki ikawa haitoshi sana watoto
wetu kuja kuwa na hofu ya Mungu pindi
watakapokuja kuwa viongozi .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE