June 12, 2017

WACHIMBAJI WAFUNIKWA NA KIFUSI NYAKAVANGALA , MAJAMBAZI WALIOWAVAMIA WAKAMATWA

Kamanda  wa  polisi  mkoa wa Iringa Julius Mjengi  akinyesha  bastola iliyokamatwa na majambazi hao  wa Nyakavangala 

                           Na MatukiodaimaBlog

SIKU  mbili  toka  majambazi  kuvamia wachimbaji    wadogo wadogo  na  kujeruhi  9 kabla ya  kuwapora  pesa  zaidi ya milioni 81 na dhahabu  gram 490   wachimbaji watatu kati ya nne katika mgodi  wa  dhahabu wa  Nyakavangala  tarafa ya  Ismani  wilaya ya  Iringa  mkoani  Iringa  wamenusurika   kifo  baada ya  kuangukiwa  na  kifusi  wakiwa  ndani ya mgodi  huo .

Imeelezwa  kuwa   mgodi huo  uliohusika  na tukio hilo ni  ule  ambao kamati ya  ulinzi na  usalama mkoa wa Iringa  iliagiza  usiendelee kufanywa shughuli za  uchimbaji  hadi  utakapoboreshwa  zaidi  kutokana na kuwepo   wahimbaji wa  mgodi huo  kuchimba bila kujengea miti kuzuia  kifusi  kuangukia ndani ya  mgodi huo .

Akizungumza na  mwandishi wa  habari hizi  kwa njia ya  simu kutoka eneo la  tukio  diwani wa kata ya   Malengamakali  Franzisca  Kalinga  alisema  tukio hilo  lilitokea majira ya saa 3  usiku wa  kuamkia  leo  na  kuwa  waliokuwemo ndani ya  mgodi huo ni  wachimbaji  wanne .

Kalinga  alisema  mgodi huo  ulikuwa  hatarini  na kamanda wa  polisi  mkoa wa Iringa Julius Mjengi na kamati  ya ulinzi na usalama  ilitoa  agizo la wachimbaji hao  kutoendelea  kuchimba hadi hapo  watakapoboresha hali ya usalama  ila  hawakuweza  kufanya   hivyo.

Alisema  hadi majira ya saa 5  asubuhi  zoezi la   uokoaji kwa mchimbaji  mmoja  aliyekuwa  chini ya  mgodi  huo  zilikuwa  zikiendelea  huku wachimbaji  watatu wakiwa  wameokolewa  salama .

Kamanda  wa  polisi wa  mkoa wa Iringa  Julius Mjengi  alithibitisha  kutokea kwa  tukio hilo na  kuwa jeshi la  polisi mara baada ya  tukio hilo  walifika  eneo la  tukio  na  wanaendelea  kusaidia  kumtafuta mchimbaji mmoja ambae bado hajapatikana na haijulikani kama  ni mzima ama  amekufa .

Mjengi  alisema  kuwa  hali ya machimbo  hayo  sehemu kubwa   si salama na  tayari  wamepata  kufika  huko na kuwapa tahadhari  wachimbaji hao kwa  kuwataka  kuzingiatia usalama   wao kwa kuhakikisha  wanaijengea  vizuri  migodi  yao kabla ya  kuingia chini  zaidi ya  ardhi  .

Wakati  huo  huo  Jeshi la  polisi  mkoa wa Iringa  linawashikilia  watu saba  wakihusishwa na tukio la uvamizi na  uporaji fedha ,dhahabu na simu  kwa  wachimbaji  wadogo  wadogo  wa machimbo ya  dhahabu ya Nyakavangala .

Kamanda  Mjengi  alisema  kuwa  tukio la  uvamizi  hilo  lilifanyika Juni 9 majira ya saa 1 usiku na  watu hao   wanaosadikiwa kuwa ni majambazi   wapatao  zaidi ya 8  waliweza  kutoweka baada ya  kufanya uporaji huo na  jeshi la  polisi  liliendelea na msako  mkali .

“majambazi hao  walivamia eneo la Krasha  ya  Paul Mkuya  na  maeneo ya  jirani na kulazimisha  watu  kulala chini  na kuanza  kuwajeruhi kwa  nyundo  na mapanga kabla ya  kufanya uporaji huo  na kufanikiwa kutoweka na pesa na dhahabu “

 Alisema  katika  tukio hilo  watu  9  walijeruhiwa maeneo mbali mbali na  baadhi yao  bado wanaendelea  na matibabu katika  Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa  na kuwa hadi sasa  jeshi la polisi limefanikiwa  kuwakamata  watu  7  wanaosadikika  kuhusika na uporaji huo wakiwemo wawili ambao  wamekutwa  na silaha  aina ya  Bastola isiyo na namba  ikiwa na magazini  moja na risasi  moja wakiwa  wanajiandaa kutoroka  eneo la Ndiuka  mjini Iringa .

Hivyo  alisema  jeshi la  polisi  linaendelea  kuwahoji  zaidi  watu hao  kabla ya  kuwafikisha mahakamani kwa   tuhuma  za  kuhusika na unyang’anyi wa  kutumia  silaha  kwenye   mgodi huo wa Nyakavangala .
TAZAMA VIDEO  HAPA CHINI 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE