June 25, 2017

WABUNGE WA CCM MKOA WA IRINGA WATOA TAMKO KWA RAIS DKt MAGUFULIWABUNGE wa chama  cha mapinduzi (CCM) katika majimbo ya mkoa wa Iringa wametoa tamko la pamoja  linalopongeza jitihada mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli.

Wametoa tamko hilo juzi huku wadau mbalimbali wa maendeleo wa mkoa wa Iringa kesho (leo Jumamosi) wakifanya maandamano ya amani kupongeza jitihada hizo.

Wabunge hao ambao wote wanatoka Chama cha Mapinduzi (CCM) ni pamoja na Godfrey Mgimwa (Kalenga), Cosato Chumi (Mafinga Mjini), Venance Mwamoto (Kilolo), Mendrad Kigola (Mufindi Kusini) na wabunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Rose Tweve na Ritta Kabati.

Wakizungumza na wanahabari wakati wakitoa pongezi hizo wabunge hao walisema anachofanya Dk Magufuli na siwa na ule msemo usemao “mwenye macho haambiwi tazama.”

 Mwenykiti wa wabunge hao wa mkoa wa Iringa, Ritta Kabati alisema; “sisi wabunge wa mkoa wa Iringa tunampongeza sana mheshimiwa Rais kwa hatua anazochukua na azma yake ya kuona rasilimali za nchi zinatumika kwa faida ya wote.”

Alisema wao kama wabunge wa mkoa wa Iringa wako pamoja na Rais Magufuli katika kulijenga Taifa linaloelekea katika uchumi wa viwanda.

Akizungumzia maandamano ya leo Jumamosi, mwakilishi wa kamati inayoratibu tukio hilo Fuad Mwasiposya alisema yanafanywa kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali wa maendeleo wa mkoa wa Iringa.

“Wapo wafanyabiashara, wanafunzi, madereva, wanazuoni na makundi mengine ya jamii ambao kwa kupitia wawakilishi wao tulikutana na kuunda kamati ya kumpongeza Mheshimiwa Rais,” alisema.

Alisema maandamano hayo yenye baraka zote za serikali ya mkoa wa Iringa yataanza saa 2.00 asubuhi katika bustani ya Manispaa ya Iringa, yatapita MR Hotel hadi katika uwanja wa Mwembetogwa yatakakopokolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza.

“Baada ya kupokelewa kutakuwepo na mada itakayotolewa na baadhi ya wahadhiri wa vyuo vikuu vilivyoko mjini Iringa itakayozungumzia historia ya vita ya uchumi,” alisema.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE