June 13, 2017

UBAKAJI WAFUNIKA REKODI YA KUJINYONGA IRINGA

                                                                       RPC Mjengi
PAMOJA na  mkoa  wa Iringa awali   ulikuwa katika  rekodi  mbaya ya  wananchi  wake  kukimbilia  kujinyonga  pindi  wanapokwazika  rekodi  hiyo  imebadilika  baada ya  kufunikwa na  rekodi mbaya  ya  ubakaji wa  watoto  .

Kamanda  wa   polisi wa  mkoa wa Iringa  Julius  Mjengi  aliueleza  mtandao  huu wa matukiodaimaBlog   kuwa  matukio ya  ubakaji  watoto   na  watu  wazima  yameendelea  kuchukua  sura  mpya  mkoani  hapa  na  kuwa  jeshi   la polisi limeendelea na msako wa  kusaka watu hao  wanaoendesha  vitendo hivyo  vya ubakaji .

Akizungumzi  watoto  wawili  mmoja wa miaka 8 anayesoma  darasa la  pili shule  ya msingi Mlangali  na  binti  wa miaka 17 mkazi wa Frelimo  mjini  Iringa  ambao  wamebakwa ndani ya  siku  mbili alisema  watuhumiwa wa  ubakaji huo  wanatafutwa ili  kufikishwa mahakamani .

Kamanda  Mjengi  alisema  kuwa  mtoto huyo wa darasa la  pili  mkazi wa Mwangata  alirubuniwa  kwa andazi na  mtuhumiwa  huyo wa ubakaji  aliyefahamika kwa  jina moja la  Adam ambaye  alipofanikiwa  kumdanganyishia andazi  mtoto huyo  aliingia  chumbani kwake na kumfanyia  kitendo  hicho cha  ubakaji .

Adam  alifanya  kitendo hicho  cha ubakaji katika  eneo la Mwangata  tarehe 4/6/2017  majira ya saa 4 usiku  ikiwa huku  vijana  wawili  ambao  wanatuhumiwa kumbaka  binti wa miaka 17 walifanya tukio hilo kwa  kupokezana huku wakiwa  wamemziba mdomo binti huyo siku ya  tarehe 5  majira ya saa10.30  jioni  eneo la njia ya  Mlima  Gangilonga  wakati binti huyo  akitokea  Ipogolo  kwa  sura  wanafahamika na  wanaendelea  kusakwa .

Hata   hivyo  alisema   watuhumiwa  hao  wanatafutwa na  jeshi la  polisi na  kuwaomba  wananchi  wenye  taarifa ya walipo  wahusika  hao kutoa taarifa  ili  wakamatwe .


Hivyo  aliwataka  wazazi  kuwa makini na  watoto wao na  kutowatuma  usiku madukani  ama  maeneo ambayo ni  hatari kwa  usalama  wao na  ikipendeza  kuanzia  saa 12  jioni  watoto wasiruhusiwe  kutoka nyumbani .

MWISHO 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE