June 11, 2017

TIMU YA BRAZIL FC NA POLISI IRINGA ZAPIGWA FAINI RITTA KABATI CHALLENGE CUP ,KWA VURUGU

Kikao  cha maamuzi kati ya  Polisi na  Brazil  kufuatia  kufanya  vurugu  uwanjani  jana
Mwenyekiti  wa  kamati ya mashindano  Gerald Malekela  kulia na katibu wake  Steven Lihawa  wakitoa majibu ya  vurugu kwa wanahabari 
Viongozi wa  timu ya  Polisi  Iringa
Mwalimu wa timu ya Polisi Iringa Sarehe Moleli

Mratibu  wa mashindano ya  Ritta Kabati Challenge Cup Fredy Mgunda (  kushoto ) akimkabidhi  mpira  meneja wa timu ya Brazil Fc  ya Msindo Mussa Isaya jana  baada ya  timu  hiyo na ile ya  polisi  kupigwa faini kwa kufanya vurugu katika mchezo  wao

 .............................................................................................................................................
                                         Na  MatukiodaimaBlog


TIMU   ya  polisi na Brazil  ambazo zinashiriki  mashindano  makubwa ya  aina yake  mkoani Iringa  ya  Ritta Kabati  Challenge Cup 2017  zimepewa  onyo kali na kamati ya mashindano hayo baada ya  mchezo  wao  kuvunjika  kutokana na vurugu  uwanjani .

 Akizungumza na wanahabari leo  katibu  wa kamati ya mashindano hayo  Steve  Lihawa  alisema  kuwa   timu  hizo   mbali ya kupewa onyo kali  ya  kutojirudia kufanya  vurugu  uwanjani  pia zimepigwa faini ya  shilingi 50,000 kila  mmoja  kabla ya  kufanya marudio ya mchezo huo   siku ya  jumanne .

Katibu   huyo  alisema  kuwa  kitendo  cha  mashabiki  wa  timu  hizo mbili kufanya  vurugu  wakati  wa mchezo huo    uliochezwa  jumamosi katika  uwanja wa Kreluu ni  uvunjaji  wa kanuni  za mashindano hayo   kanuni  ambazo kila  timu shiriki   katika mashindano hayo  ilikabidhiwa  na  ilipaswa  kufuata  kanunu  za  mashindano hayo .

Alisema  kuwa  lengo la kuanzishwa kwa mashindano hayo  na mbunge wa  viti maalum mkoa wa Iringa kupitia  chama  cha mapinduzi  (CCM ) Ritta kabati ni  kutaka  kuona  vipaji vya vijana  katika  michezo  zinaonekana na kuwawezesha  kupata  ajira  kupitia  klabu mbali mbali na  sio kuona  mashindano hayo yanakuwa uwanja wa  vurugu .

Lihawa  alisema  kuwa mchezo huo  uliovunjika kati ya  polisi Iringa na  Brazil  ya  Mshindo  ndio ulikuwa  ni  mechi ya  mwisho  katika mzunguko wa kwanza  kwenye mashindano hayo ila  kutokana na  vurugu  hizo timu   hizo  zilivunja kanuni ya  sita ya mashindano ambayo  inatamka  wazi kuwa kamati  inaweza kuitoa  katika mashindano  timu  yoyote inayotishia  usalama  wa mashindano hayo  huku kanuni ya  10  timu itakayosababisha  mchezo kuvunjika ama kuvunjwa  itaondolewa katika mashindano hayo .

Hivyo  alisema  kuwa  kuvunjika kwa mechi  hiyo ni  wazi timu  zote  zilipaswa  kuondolewa katika mashindano hayo ambayo  yalianza na  timu 43  ila  busara ya kamati ya  mashindano imetumika na kuwapa adhabu ya  kulipa faini  ya shilingi 50,000 kwa  kila   pande na tayari  timu ya polisi Iringa  imelipa faini na bado  timu ya Brazil  ambayo  itapaswa  kulipa faini  hiyo kabla ya  mchezo kuchezwa  vinginevyo itakuwa  imejivua katika mashindano hayo .

“ Kanuni  za mashindano haya ni zile  zinazohusika katika  mashindano ya  ngazi ya  wilaya na mkoa hivyo timu  ikifungiwa kuendelea na mashindano  hayo itakuwa  imejitoka katika mashindano mengine yakiwemo ya  wilaya  na mkoa “

Mwalimu  wa  timu ya polisi   Sarehe Moleli  alisema  kuwa  wamepokea adhabu  hiyo na kuomba radhi kwa yote yaliyotokea na  kuwa  wakati  vurugu  hizo zinatokea  timu yake  ilikuwa  mbele  kwa magoli  mawili  huku  wapinzani  wao  wakiwa hawajapata  goli na  kuwa chimbuko la vurugu ni  kufungwa na  ndipo  walipompiga mmoja kati ya  wachezaji wa  polisi  ila wao kama  polisi  wapo  tayari  kuendelea na mashindano hayo na hivyo  wamelipa faini  hiyo  kama  walivyoagizwa .

Hata  hivyo  alitaka  waamuzi waliochezesha mchezo huo  kutochezesha  mchezo  wao  wa marudiano kwani ndio chimbuko la  vurugu  hizo.

 Hasan Saidi  ambaye ni  msemaji wa  timu ya  Brazil  alisema kuwa  walilazimika  kufanya  vurugu  kutokana na  wapinzani  wao  kuonyesha kuwa na dalili za vurugu  na kuwa  kutokana na msamaha walioupata  hawapo tayari  kufanya  vurugu   tena na  watazingatia kanuni  za mashindano hayo .

Mwenyekiti wa mashiindano  hayo Gerald  Malekela alisema hadi sasa mzunguko wa kwanza  unataraji kukamilika  jumanne kwa Polisi na  Brazil  kurudiana na  baada ya hapo mzunguko  wa pili  utaendela na  kuzitaja timu  zilizoingia  hatua ya pili ya mzunguko  huo kuwa ni kwa  kundi  A ni Kihesa   FC,  Ilala, African Boys , Black Cheeter , Boda boda, Magereza   wakati kundi B ni  Itagutwa , Ifunda ,Kitowo, Ngangilonga , River Hood , na Malingumu .0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE