June 23, 2017

THRDC WALAANI MAUWAJI YA ASKARI KIBITI

MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA

TAMKO KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TUKIO LA KUUWAWA KWA POLISI WAWILI, KIBITI- MKOA WA PWANI


Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania wenye wanachama zaidi ya 130 tunalaani vikali mauaji ya kutisha ya polisi wawili wa kikosi cha usalama barabarani katika eneo kati ya Bungu na Jaribu katika Wilaya ya Kibiti, Mkoa wa Pwani.

Taarifa zinaonyesha kwamba muda mfupi baada ya vifo vya polisi wa usalama barabarani waliotajwa hapo juu, gari lao na pikipiki vilichomwa moto kabla ya majambazi hao kutokomea mahali kusikojulikana.

 Tukio hilo la kutisha lilifanyika tarehe 21 Juni 2017 wakati polisi wa usalama barabarani walipokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kila siku. Ripoti kutoka kwa Jeshi la polisi iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani Onesmo Lyanga ilithibitisha vifo vya Polisi hao wa usalama barabarani ambao majina yao ni Sajini Salum na Konstebo Masola.


Ongezeko La Mauaji Ya Askari Pwani
Kumekuwa na matukio mengi ya mauaji ya polisi na raia ambayo yanaathiri usalama wa kila raia na taifa kwa ujumla.

 Ni wazi kwamba matendo ya polisi kuuawa sasa yameongezeka kutokana na ukweli kwamba ni Aprili 13, 2017 tu, polisi nane waliuawa katika Mtaa wa Mkengeni, Kijiji cha Uchembe, Kata ya Mjawa, Wilaya ya Kibiti katika Mkoa wa Pwani.

Maofisa wapolisi hao walipigwa risasi na Majambazi wakati wa kujiandaa kuondoka kutoka kwenye kizuizi cha barabarani kuelekea kituo cha jirani cha Polisi.


Takwimu zinaonyesha kwamba, tumepoteza maafisa wa polisi 10 ambao wameuwawa kwa risasi Wilayani Kibiti ndani ya kipindi cha miezi miwili iliyopita. Takwimu hizi zinashangaza hasa wakati ambapo tukilinganisha idadi ya maafisa wa polisi kwa sasa na idadi ya raia kila polisi anaopaswa kuwalinda.

Mbaya zaidi, muda ambao matukio haya mabaya yamefanyika ni mfupi sana wakati mtu angeweza kutarajia ufumbuzi wa haraka wa tatizo muda mfupi baada ya mauaji ya tarehe13 Aprili 2017.

Kwa hiyo ni dhahiri kwamba, usalama wa wananchi wengi ambao wanategemea maafisa wa polisi tayari umekuwa hatarini.


Matukio ya mauaji ya Kibiti yameelekezwa sasa mpaka kwa raia ambao wakati kwa muda sasa wamefanyiwa ukatili na hatimaye kuuawa na majambazi wasiojulikana.

 Ndani ya wiki tatu, ripoti za mauaji ya wananchi sita zimetolewa wakati hakuna sababu zozote za msingi zilizotolewa kuhusu mauaji hayo.

 Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania kama shirika mwamvuli la kutetea watetezi wa haki za binadamu Tanzania lilitoa tamko kulaani mauaji hayo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kukabiliana na hali hiyo.


Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania kama shirika mwamvuli la kutetea watetezi wa haki za binadamu Tanzania imekuwa ikitoa matamko kulaani mauaji haya ya polisi  na kushauri hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kukabiliana na hali hiyo lakini bado tunashangaa kuona mauaji yakiendelea
Tunapotambua jitihada za kukabiliana na hali ambayo Polisi wetu na Jeshi la Ulinzi, miongoni mwa wengine inachukua, tunaamini kamba hatua nyingine za kibunifu na za haraka ni muhimu kuchukuliwa wakati huu.

 Nchi yetu imekuwa kisiwa cha amanina matukio machache    na mabaya kama haya huweza ondoa sifa hii. Kwa hiyo ongezeko la matukio haya itakua ni ishara ya kupoteza  ikiwa hatua za dharura na madhubuti hazitachukuliwa.


Madhara ya Mauaji ya Polisi Kwa Jamii
Polisi, hususani wale wanaofanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na taaluma ni watetezi wa haki za binadamu na sisi kama watetezi wa watetezi wa haki za binadamu ni wajibu wetu kukemea na kulaani kwa nguvu matukio ya mauaji ya polisi ambao ni walinzi wa Haki za raia na mali zao.


Matukio haya huleta hofu kwa watu ambao wanategemea Polisi kuwalinda raia na mali zao.

Ikiwa hatua za upelelezi za kuchunguza majambazi hawa hazitachukuliwa, kuna hatari kubwa kwa usalama wa nchi na raia wake.

 Kwa hiyo, serikali na umma kwa ujumla inakumbushwa wajibu wao wa kutambua na kuondosha wahalifu wowote ili nchi yetu iendelee kubaki salama.

Kama kauli mbiu ya Mtandao wetu inavyosema "Ni bora Mteteziwa Haki za Binadamu abaki hai kuliko kufa".

Vile vile kauli mbiu ya "Polisi wanapaswa kuendelea kuishi ili wananchi wawe salama" inafaa kuheshimiwa wakati huu ambapo polisi wengi wanaonekana kuwa hatarini.

 Ni lazima ieleweke kwamba "usalama wa maafisa wa polisi ni usalama wa Wananchi" ili waweze kuendelea na majukumu yao ya kulinda raia na mali zao.

Sababu Zinazosababisha Kujirudia kwa Matukio Haya
Mtandao unapendakusisitiza sababu zinazosababisha matukio haya zisipotatuliwa matukio haya yataendelea kujirudia.

Sababu hizoni pamoja na haya yafuatayo:

• kuwepo kwa mazingira magumu ya kufanya kazi kwa maafisa wa polisi kuanzia kuwepo kwa nyumba duni, vifaa na ukosefu wa magari.

• Kuwepo kwa uhusiano mbaya kati ya wananchi na Jeshi la Polisi hasa kutokana na vitendo vingine vya kutumia nguvu kupita kiasi ambavyo wakati mwingine hutumiwa vibaya au polisi kunyanyanyasa raia na wakati mwingine huwaua.

Ikumbukwe kwamba uwezo wa Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu hutegemea uhusiano wake na umma.

• Jeshi la Polisi bado linatumia mbinu za zamani katika ufuatiliaji naufanyaji wa shughuli zake.

Wanapaswa kuwa na vifaa vya kisasa ambavyo vinaweza kuchunguza aina zilizopo za silaha za mpinzani katika umbali wa kilomita kadhaa ili kujilinda.

• Jeshi la Polisi bado hawana mfumo wa kujitegemea ambao utafanya raia wa imani zote waweze kushirikiana.

Uhuru wa Jeshi kutoka kwa mikono ya viongozi wa kisiasa inaweza kurejesha ushirikiano na wananchi kwa asilimia kubwa na hatimaye kuboresha ulinzi na usalama wa polisi.

• Katika taifa letu hasa katika maeneo ya miji, hakuna vifaa sahihi kama kamera za mitaani (CCTV-Kamera) ambazo zinaweza kutambua yote yanayotokea mitaani. Kuwepo kwa kamera hizi kutasaidia Polisi kutambua wahalifu.

Pia wakati matukio haya yanapojitokeza, jitihada/hatua ambazo zinachukuliwa zinaonekana kuwa za  muda mfupi na sio za kudumu na hiyo ndiyo sababu ya matukio hayo kujirudia.

Wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania tunatoa pole kwa jamaa za wale ambao wamepoteza maisha yao lakini pia kwa Jeshi la Polisi na jamii kwa ujumla kwa kupoteza wapendwa na nguvu kazi ya taifa.

 Tumepoteza watu muhimu ambao huduma yao ilikua bado inahitajika hasa katika kipindi hiki ambapo matukio mbalimbali ya kutisha yanajidhihirisha ikiwa ni pamoja na kutoweka kwa raia na mali zao kunakoendelea kuenea nchini.

WITO WETU
Serikali kupitia wizara husika inapaswa kuchukulia jambo hili kwa msisitizo mkubwa na kuongeza jitihada zaidi katika kufanya uchunguzi wa kina  ili kutambua wahalifu wa matukio ya mauaji ya polisi na raia ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Tunaiomba serikali iruhusu wajumbe na wanachama wetu kufanya maandamano ya amani nchini kote ili kulaani mauaji haya ili sauti za watetezi ziweze kusikika na kuenea sana katika vita dhidi ya mauaji haya.

Ni wakati  sahihi sasa kwa wananchi kujiunga kwa pamoja kufanya juhudi  katika kupambana na matukio mabaya ya namna hii. Tunaamini kwamba majambazi hawa ni watu wanaoishi na raia wa kawaida mitaani na ili kujua ni mahali gani  au ni nini wanachofanya tunahitaji kufanya kazi ya pamoja  ambayo itakua kamilkifu na watu wote katika kupambana na vita hii.

Mbinu za siri  na ubunifu zinapaswa kutumika katika vita hivi ili kuhakikisha maadui hawatambui njia yoyote inayochukuliwa dhidi yao.

Ni ukweli usiopingika kwamba shughuli zinazoendelea na mipango dhidi ya maadui  hawa ambao huwaua watu wetu kwa kiasi kikubwa zimegundulika na kuwafanya maadui kujiandaa dhidi ya wapinzani wao.

Matukio kama haya hayapaswi kuhusishwa na  masuala ya kisiasa.

 Hivyo, sisi kama taifa tunapaswa kuungana na kuacha ushirika wetu wa kisiasa na kupambana na matukio kama haya yanayotishia amani dhidi ya watu na taifa kwa ujumla.

Serikali inapaswa kutoa motisha au tuzo kwa watu wote watakaoweza kutoa taarifa ambayo zitasababisha  kukamatwa kwa wahalifu wa tukio hili baya.

Majeshi yote nchini Tanzania wanapaswa kuendelea kuungana   kwa pamoja  katika kufanya shughuli za uchunguzi kina ili kutambua  mtandao wa wahalifu na kukamatwa  kwa majambazi wote nchini Tanzania.

Jeshi la polisi linapaswa kuendelea kutimiza majukumu yake ya kisheria, kitaaluma, kwa ufanisi  ili kuondoa taswira  iliyojengeka kwa wananchi  ambao wanaona polisi kama  maadui zao.

Kamera za mitaani zinapaswa kuwekwa mitaani katika miji  ili  kusaidia kuweza kuwatambua  wahusika wa uhalifu
Jeshi la polisi linapaswa kufanya maboresho kwa kutumia mbinu za kisasa wakati wanaendesha doria ili waweze kutambua matukio kabla ya kujitolea.

Jeshi la polisi linapaswa kuimarisha uhusiano wake   na wananchi kwa kuondoa hali zote zinazoweza  kuchangia  kupoteza ushirikiano huo.

Wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania tunatoa pole kwa jamaa za wale ambao wamepoteza maisha yao lakini pia kwa Jeshi la Polisi na jamii kwa ujumla kwa kupoteza wapendwa na nguvukazi ya Taifa.

 Tumepoteza watu muhimu ambao huduma yao ilikua bado inahitajika hasa katika kipindi hiki ambapo matukio mbalimbali ya kutisha yanaonyesha kutoweka kwa raia na mali zao zinaendelea kuenea nchini.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania unaungana na familia, jamaa , marafiki, Jeshi la polisi pamoja na Serikali kwa ujumla  katika wakati huu mgumu  ambao Taifa linaomboleza  vifo vya wapendwa wetu ambao wamefariki.

ROHO ZAO ZIPUMZIKE KWA AMANI……………….AMINA.
Imetolewa leo mnamo tarehe 23 Juni 2017

………………………………………………………………….
Na Onesmo Olengurumwa
Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE