June 12, 2017

TEMBO WAUA MWANANCHI MMOJA IRINGA

TEMBO  wa  hfadhi ya  taifa ya  Ruaha   asababisha   kifo  cha  mazi  mmoja wa  Kisinga  Nguna  aliyefahamika kwa jina la Daud  Kaluku  (50) .

Taarifa  iliyothibitishwa na  mwenyekiti wa kamati ya  uinzi na  usalama  wilaya ya  Iringa  mkuu wa  wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  kwa  mtandao huu wa matukiodaima inaeleza kuwa  tukio hilo limetokea leo majira ya  saa 9 Alasiri .

Kuwa  jana  baada ya  Tembo  kuongezeka katika  eneo hilo  askari  wa hifadhi ya  Ruaha  walifika  eneo hilo ili  kukabiliana na  Tembo  hao ambao  walikuwa  wengi  zaidi .

"Tumeendelea kupambana na tembo hawa lakini kutokana na wingi wa tembo hawa Askari wetu wa wanyama pori wanazidiwa"

Alisema  kuwa wingi wa tembo hawa unasababishwa na Tembo hawa kukosa maji hivyo wengi wao kuyatafuta maji   nje ya hifadhi na kuwa  kuna mafanikio makubwa ya kuzuia ujangili yamesababisha idadi kuongezeka kuendelea  kuongezeka  zaidi .

"Tumejaribu kutumia mabomu ya kelele ili kuwarudisha lakini bado ni changamoto kubwa.nawaomba wananchi wawe makini sana hasa wanapo ona kundi la Tembo....hadi sasa Tembo wanaendelea kuaharibu mazao maeneo ya tarafa za Pawaga, Idodi na Ismani"  alisema  mkuu  huyo wa  wilaya

Kuwa  wanaomba  wizara ya  maliasili  kusaidia  kuongeza  nguvu ya  askari  zaidi  ili  kuwafukuza  Tembo  hao na  kuokoa uhai wa wananchi pamoja na usalama  wa mazao  yao.


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE