June 4, 2017

NAIBU KATIBU MKUU CCM MPOGOLO AWAPA SOMO WASOMI

Mgeni  rasmi  katika mahafali ya  wanachuo  Iringa ,naibu katibu  mkuu wa CCM bara Rodrick Mpogolo wa  nne kulia  akiwa na  viongozi  mbali mbali  akiwemo mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na viongozi wengine  wakati  wakipiga picha ya  pamoja na wahitimu 
Mpogolo  akigawa  vyeti kwa  wahitimu
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza  akitoa  salam zake
Mpogolo  akipokelewa na  wanafunzi  wa  vyuo Iringa
Mjumbe  wa kamati ya  siasa  mkoa  Joseph Muhumba  akisalimiana na naibu katibu  mkuu
katibu  msaidizi wa wilaya ya  Kilolo  akisalimiana na Mpogoo
RC  Masenza  akimpokea  naibu katibu  mkuu
Wanachuo  wakifurahi  pamoja na  viongozi  mbali mbali


Katibu  wa  UVCCM mkoa wa Iringa James  Mgego  akitoa  taarifa ya  UVCCM

Mkuu wa  wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  akisalimia
Katibu  wa  CCM Iringa  vijijini Bw  Dodo  akitoa  salam  zake

Mhitimu  Bether Mpeli  Mwaisumbi  akifurahi kuwa  CCM


RC  Masenza akifurahi na wahitimu

Msanii  mwanachuo  wa  RUCU Jenipher George  akionyesha uwezo  wake wa  kucheza na moto

Na  MatukiodaimaBlog
UTUMBUAJI  wa  majibu na  ufukuzaji  wa wasaliti  wa uchaguzi mkuu mwaka 2015 wa  chama  cha  mapinduzi  (CCM)  uliofanyika mwaka  huu na  chama   hicho Taifa umepelekea  ofisi ya jumuiya ya  umoja  wa  vijana (UVCCM)  mkoa na wilaya ya  Iringa mjini  kuendeshwa na makatibu  pekee .

Katibu  wa UVCCM mkoa  wa  Irina  James  Mgego  aliyasema  hayo  jana  wakati  akimkaribisha naibu  katibu  mkuu wa CCM  Tanzania  Bara  Rodrick  Mpogolo  kuwatunuku  vyeti wana  CCM wakati wa mahafali ya  wanachuo  hao yaliyofanyika  ukumbi wa siasa ni  kilimo mjini  hapa .

Mgego  alisema  kutokana na kufukuzwa kwa viongozi wasaliti  ndani ya  chama hicho na kusimamishwa  kwa baadhi yao  ofisi  za  UVCCM mkoa na ile ya Iringa  mjini  zinaongozwa na makatibu  pekee  huku  wajumbe na  waliokuwa  wenyeviti wa  jumuiya   hizo  kukumbwa na fagio  la  usaliti.

Hata  hivyo  alisema  bado  shughuli  zote  ndani ya  jumuiya  hizo  zinakwenda kama kawaida  na kuwa  wakati huu ambao  wanaelekea  kwenye chaguzi ndani ya  chama wanaendelea  kuwachunguza baadhi ya  wana CCM  wakiwemo vijana  ambao  wanazunguka mitaani na  waliotumbuliwa kutaka  kuhujumu uchaguzi huo na  wakibainika  nao  watachukuliwa hatua  kali .

Mkuu  wa mkoa  wa  Iringa Amina Masenza  alisema  kuwa ili  umoja  huo wa  vijana  uzidi kuwa na nguvu  ni  lazima  vijana  hao  kuungana  na  kuepuka kutumiwa na  baadhi ya  watu wasiopenda  kazi nzuri  inayofanywa na mwenyekiti wa CCM Taifa  Rais  Dkt  John Magufuli ya  usafishaji wa  chama  hicho kwa kuwaondoa  wasaliti .

Kwani  alisema hata  penda  kuona  vijana  hao  wanatumika  vibaya  kuvuruga  chama na  kuwa  wakibainika  wanapaswa  kushughulikiwa  vilivyo  bila  kuwaonea  haya  na kama ni  noma  na iwe  noma ila lazima  wasaliti  wawajibike .

Masenza  alisema  kuwa  sababu ya  chama  kupoteza  jimbo la Irina  mjini ni  usaliti  uliofanywa na wana CCM na  baadhi ya  viongozi kwa uchu  wa  madaraka waliokuwa nao na  kuwa   ili  kukifanya  chama   hicho  kuwa chama  cha  kuaminika kwa  wananchi  wote  ni lazima kuwa pamoja na  wana CCM  kuondokana na tabia ya majungu  na  ubaguzi .

Kwa upande  wake naibu  katibu  mkuu CCM Bara Mpogolo  alisema  kuwa bado hakuna chama  chenye nguvu ya  kumshinda   Rais Dkt  Magufuli mwaka 2020 hivyo kazi  ya  ushindi  wa uchaguzi  huo inapaswa  kufanywa na  vijana huku akiwataka   wasomi  wa  vyuo  vikuu hapa  nchini   wakati   wakisubiri  nafasi  za ajira  serikali  kujiunga  katika  shughuli  zao  binafasi  zikiwemo  za  kilimo .

Mpogolo alisema  kuwa  chama  chake  hakipendezwi na tabia ya  baadhi ya  wasomi  kushinda  vijiweni  na  kufanya maandamano wakati  kupitia  elimu  waliyoipata  wanauwezo  wa  kujiajili  wenyewe  katika  sekta  zisizo  rasmi .

  Wasomi  wa CCM tunataka  msiwe  kama  wasomi wa vyama  vya  upinzani  ambao  wao  kazi yao kubwa ni  kupinga na kulalamika  kila  jambo …..wewe ni msomi  ukishatoka  chuo  tafuta  kazi ya kufanya  hata  ya  kwenda  kupanda  miti ama  kilimo huku  ukisubiri maombi  yao  ya kazi sio  kwenda  kushinda  vijiweni  bila  kazi”

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE