June 12, 2017

SERIKALI ZOTE MWANACHAMA AEC ZATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI KTK TAFITI ZA KISAYANSI

Na Hellen .I. David-Dar es Salaam

SERIKALI  za Ukanda  wa Afrika Mashariki hususani Kenya,Uganda na Tanzania ikiwa moja wapo  zimetakiwa kuweka mazingira mazuri ya kisera hasa katika Tafiti mbalimbaliza kisayansi ambazo zipo ili kuwafikia wakulima nao waweze kunufaika na kilimo.

Hayo yamebainishwa na watafiti kutoka Tume ya sayansi na teknolojia (COSTECH) na Taasisi ya Teknolojia ya Kilimo Afrika wakati walipotembele mashamba ya wakulima wa Mihogo,Mahindi pamoja na pamba katika mkoa wa Mwanza hivi karibuni.

Watafiti hao walisema kuwa magonjwa yanayoikumba Tanzania hasa katika zao la mihogo  magonjwa ya batobato kali na Michirizi ya kahawia ni magonjwa ambayo yapo nchi zote tatu.

“Magonjwa hayo yapo hata Uganda lakini upande wetu ni hatari Zaidi kwani yote mawili yanatokea katika mmea mmoja,hivyo anaziomba serikali za nchi zote kuangalia namna ya kuweza kuachia mbegu zilizopo zinawafikia wakulima kwa wakati wakati wanasayansi wanaendelea kufanya utafiti wa mbegu bora zitakazo weza kumaliza hilo tatizo kabisa,”Alisema Mtafiti kutoka Uganda Philip Chemonge
Aidha kwa upande wa Kenya nao wanalalamikia ugonjwa huo wa batobato kali pamoja na michiriki ya kahawia katika zao la mihogo.

“Hali hii ya magonjwa hata Kenya ipo ambapo kama mtaalamu nilijaribu kulima shamba la mihogo ili iwe shamba darasa kwa wakulima lakini shamba lote lilipata ugonjwa huo na kukosa kuonyesha mfano kwa wakulima,hivyo serikali zinahitajika kuhakikisha tafiti zilizopo zinafikia wakulima kwa kuwa zimeshaonyesha hali ya kukubaliana na magonjwa hayo ili kuepukana na njaa,”Alisema Meneja Mpango wa OFAB-Africa katika Teknolojia ya Kilimo Afrika Foundatio Daniel Otunge

Kwa upande wake Mshauri wa Jukwaa la Ofab nchini na Mtafiti toka Tume ya sayansi na Teknolojia Dkt Nicholaus Nyange alisema kwamba jitihada watakazo chukua sasa kwa ajili ya kupambana na magonjwa ni kuanza  kutoa elimu kupitia mashamba Darasa watakayo panga ili njia nzuri ya kutumia mbegu  zinazovumulia magonjwa hayo ifahamike kwa wakulima.

“Kuanzia mwezi wa tisa tutachagua wakulima ambapo tutakuwa na mashamba maalum ya mfano katika kufundishia kwa ajili ya aina ya mbegu zilizoonyesha kuvumilia magonjwa hayo ya batobato na michirizi ya kahawia pamoja na mashamba hayo tutakuwa na mashamba kwa ajili ya kuzalisha mbegu hizo ili kuhakikisha mnapata hizo mbegu na msimu ujao wa kilimo basi muanze kulima polepole aina zinazovumilia magonjwa hayo” Alisema Dkt Nyange.

Hata hivyo bado jitihada zinatakiwa kwa serikali kuweka kanuni za tafiti za kisayansi vizuri ili kumsaidia mkulima katika kupambana na magonjwa ya mazao pamoja na ukame ambao unasababisha njaa katika Taifa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE