June 6, 2017

RC OLE SENDEKA ATAKA WANASIASA KUTOWALINDA WANAOHARIBU MAZINGIRA

Mkuu  wa  mkoa wa Iringa  Amina Masenza  akishirikiana na mkuu wa mkoa wa  Njombe Christopher  Ole Sendeka  kupanda  mti  siku ya kilele  cha mazingira  duniani kilichofanyika  mkoa wa Mbeya kwa  mikoa ya  Iringa ,Njombe na Mbeya 

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza  kulia na mkuu wa wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah  wakimpongeza mwananchi wa  kilolo aliyeshinda tuzo za TANAPA 

Mkuu wa mkoa wa Njombe Sendeka  kulia akipongezwa na mkuu wa  mkoa wa Mbeya Amos Makala 

Wasanii  wakitoa  burudani  wakati wa  kilele cha mazingira 

Kikundi cha  Skauti Mufindi  wakipewa  tuzo kwa  kuelimisha jamii 

Wageni  wakiwasili  eneo  la tukio 

Mkuu wa mkoa wa Mbeya   Amos Makala   kulia  akiwaeleza jambo  mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na meneja ujirani mwema Tanapa  Ahmed Mbugi  


RC  Njombe  Christopher  Ole Sendeka  akitoa  salam  zake 
RC  Iringa  Amina Masenza  akitoa  salam 

Moronda  Moronda  kutoka  Tanapa  akitangaza   washindi wa  Tuzo DC  Kilolo Asia Abdalah kushoto na mkuu wa  mkoa Iringa wakipongeza shule ya Msosa kwa kushinda Tuzo ya  TANAPA  Na MatukiodaimaBlog
MKUU wa  mkoa  wa  Njombe Christopher Ole  Sendeka  amewataka  wana siasa  nchini  kuacha  kuwatetea  wananchi  wanaolima  kwenye vyanzo vya maji  kwa  kuhofia  kurudi  tena  katika nafasi  zao za  uongozi kwenye uchaguzi ujao wa  2020.

Akizungumza  wakati wa  siku ya mazingira  duniani na  utoaji wa  tuzo za  mazingira za   TANAPA   zilizofanyika  katika  kijiji  cha Mabadaga  wilaya ya  Mbarali  mkoa wa Mbeya kwa  mikoa  mitatu   ya  Iringa ,Mbeya na  Njombe ambayo  inachangia uhifadhi wa  mto  Ruaha  na hifadhi ya  Taifa ya Ruaha  alisema  kuwa  lazima  wananchi  waelimishwe  kuachana na  kilimo  kinachohatarisha  usalama wa mto  Ruaha  mkuu na kazi  hiyo ifanywe  na viongozi  wote  wakiwemo  wana siasa .

Sendeka  alisema  kutokana na  hali  iliyopo kwa sasa  kwa baadhi ya  wanasiasa  kuonyesha  kuanza  kuwatetea waharibifu wa mazingira  hao  wakiwemo  wanaolima katika  maeneo  oevu ni  vema  wakuu wa  wilaya  na   wakuu wa mikoa ya Iringa , Njombe na Mbeya  kuungana  kutoa  elimu  ya uhifadhi wa mazingira  pamoja na  kuwachukulia hatua wote  wanaoendelea  kuharibu  vyanzo vya maji .
“ kauli  mbiu  yetu  mwaka  huu inasisitiza  uhifadhi wa  mazingira  kama  muhimili  wa Tanzania ya viwanda  hivyo  napenda kuwataarifa  kuwa  serikali  inasisitiza  kufanya mambo  yafuatayo kama  kuzingatia  sheria za uhifadhi wa mazingira , uchomaji  wa moto na sheria  nyingine  ….sheria  zipo  jukumu  letu  kusimamia sheria  ama  kuendelea  na siasa juzi  nilikuwa Mtera  Iringa  watu wanalima kwenye  Bwawa la  Mtera  ila ukiwauliza  wanaleta  siasa “

Hivyo  alisema  iwapo  sheria  zitaachwa  bila  kusimamiwa  vilivyo wananchi hao  wataendelea kufanya   uharibifu wa mazingira  na  kuwa  kinachotakiwa  ni  kuchukua  hatua kali kwa  wanaovunja sheria   hizo  ili  iwe  fundisho kwa wengine .

Mkuu  huyo wa mkoa  alisema  ili  kufanikisha  zoezi  la uhifadhi wa mazingira  ni  lazima  kutenga  fedha za  kutosha kwa  ajili ya utoaji  wa elimu ,kusimamia sheria  hizo  ,kasi ya ushirikiano baina ya  hidafhi na wadau  wote  kutekeleza  mkakati wa Taifa wa  uhifadhi wa mazingira ,kilimo  kisichoendelevu kwenye miteremko ya milima  na vyanzo vya maji lazima vipigwe  marufuku .

Aidha  alitaka wananchi  wote  kushiriki  kuthibiti  mianya  ya  uharibifu wa mazingira  katika maeneo yao  ikiwa ni pamoja  na  kuepuka  kuchunga  mifugo katika  hifadhi na  kupiga  vita  vitendo  vyote  vinavyochangia  mazingira  kuharibika  zaidi ni  kuendelea  kupanda  miti  rafiki na  mazingira .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE